IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Rais wa Iran awatumia salamu za pongezi viongozi wa nchi za Kiislamu kwa kuanza Ramadhani

6:15 - March 24, 2023
Habari ID: 3476751
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia salamu za pongezi viongozi wa nchi za Kiislamu kwa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika salamu hizo tofauti kwa viongozi wa nchi za Kiislamu, Rais Raisi amewatakia kheri na baraka kwa mnasaba wa kuanza mwezi huu mtukufu.

Baadhi ya viongozi walionyooshewa mkono wa pongezi na Rais wa Iran kwa kuanza Ramadhani ni wa nchi za Iraq, Uturuki, Saudi Arabia, Pakistan, Tajikistan, Uzbekistan, Syria, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu, Kuwait, Qatar, Kazakhstan na Kyrgyzstan.

Rais Raisi amewaasa viongozi hao wasimame imara kukabiliana na njama za maadui za kuanzisha migogoro bandia kwa lengo la kuudhofisha ulimwengu wa Kiislamu na kueneza chuki dhidi ya Waislamu.

Jana Alkhamisi tarehe 23 Machi, ilikuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani hapa nchini Iran na katika nchi nyingi za Kiislamu kwa mwaka huu wa 1444 Hijria.

Waislamu katika nchi nyingi za Kiislamu katika eneo la Asia Magharibu (Mashariki ya Kati) na katika maeneo mengine ya dunia wameanza kutekeleza ibada ya Saum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani leo Alkhamisi.

Katika kubainisha utukufu wa mwezi huu, Mtume Muhammad SAW amesema, siku za mwezi wa Ramadhani ndizo siku bora zaidi kuliko siku nyingine zote na kuwataka Waislamu wachume na kufaidika kutokana na fadhila na baraka za mwezi huu.

President.ir

captcha