IQNA

Historia na Turathi

Oman yazindua ujenzi wa mnara wa kumkumbuka Admeri Muislamu wa China, Zheng He

13:49 - June 03, 2023
Habari ID: 3477091
TEHRAN (IQNA)- Ujenzi wa Mnara wa ukumbusho wa admeri maarufu Muislamu wa karne ya 15 miladia, Zheng He, ulizinduliwa Alhamisi katika mkoa wa Dhofar nchini Oman.

Mnara wa ukumbusho wa urefu wa mita kumi utajengwa katika mji wa pwani wa Salalah na utakuwa na umbo la meli kubwa zaidi katika msafara wa meli za He, ambay ilikuwa kubwa kushinda meli zote za Ulaya wakati huo. Mnara huo unaaashiria urafiki wa jadi kati ya Muscat na Beijing na ni matokeo ya ushirikiano kati ya ubalozi wa China na Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman.

Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi wa China nchini Oman, Li Lingping alisema: "Safari za Zheng He kwenye Bahari ya Magharibi zilichochea mawasiliano ya kirafiki kati ya China ya kale na nchi za pwani ya Bahari ya Hindi. Safari hizi ziliwezesha uhusiano wa kiuchumi, kibiashara na kiutamaduni kati ya China. na mataifa haya."

Khalid Bin Salim Al-Saeedi, mwenyekiti wa Jumuiya ya Urafiki ya Oman-China, alisema katika hotuba yake kwamba Mnara wa Makumbusho wa Zheng He unaonyesha mabadilishano ya muda mrefu na yasiyokatizwa kati ya ustaarabu wa Oman na China. Viongozi wa nchi zote mbili wamejitolea kwa maendeleo na ukuaji wa uhusiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali, alisema.

Kwa mujibu wa gazeti la Muscat Daily, mnara huo umechorwa na Taasisi ya Usanifu Majengo ya Beijing, umechochewa na 'Njia ya Hariri ya Baharini, ambayo Zheng He alitumia katika safari zake.  Zheng He alikuwa mvumbuzi na mwanadiplomasia wa zama za watawala wa Ming aliongoza meli kubwa kuelekea magharibi mara saba hadi Kusini-mashariki mwa Asia, Asia ya Kusini, Asia Magharibi na Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na kufika Dhofar mara nne. Imesemekana pia kwamba "aligundua" Amerika zaidi ya miaka 70 kabla ya Christopher Columbus mnamo 1492.

China na Oman zilianzisha ushirikiano wa kimkakati mwaka 2018 na kusaini mikataba ya ushirikiano chini ya Mpango wa Ubunifu wa Barabara ya Hariri (BRI), unaojumuisha Njia ya Hariri ya Baharini.

4145326

captcha