
Watu wetu walianza kuuliza kuhusu wakati ambapo uongozi wa kisiasa wa PA utachukua jukumu lake la kisiasa, kimaadili na kitaifa, DFLP ilisema katika taarifa.
DFLP pia iliuliza; Je, ni lini (PA) itawalinda Wapalestina na heshima yao ya kitaifa dhidi ya mashambulizi ya kikatili ya walowezi, ambayo yamekuwa jambo la kila siku kwa kuungwa mkono kikamilifu na vikosi vya Israel vinavyokalia kwa mabavu?
Kwa mujibu wa taarifa ya DFLP, matukio katika miji ya Palestina ya Turmus Ayya, Huwwar, Orif, Saanjal na mingineyo yanaonyesha kwamba kuna sera mpya ya uvamizi inayotekelezwa huko.
DFLP inaamini kuwa sera hii imejikita katika kuachilia mikono ya walowezi kuchoma nyumba, magari na mali nyingine za Wapalestina ili kuweka hofu miongoni mwao ili kurudia kile kilichotokea mwaka wa 1948.
Katika taarifa hiyo, DFLP imekariri kuwa Wapalestina wanatambua malengo ya sera hiyo ya Israel na kusisitiza; Wapalestina wanafahamu hili na hali ya mwaka 1948 haitarudiwa tena, lakini hii haiondoi (PA) katika jukumu lake la kuwatetea Wapalestina.
(DFLP) pia ilitoa wito kwa (PA) kutoamini kuwa inafanya kazi vya kutosha wakati inaitaka utawala wa Marekani kuishinikiza Israel kusitisha mashambulizi yake, ikibainisha; Huu ni mchezo wa kipuuzi.
(DFLP) ilitoa wito kwa (PA) iwageukie watu wa Palestina na kupitisha muqawama wa wananchi na wenye silaha dhidi ya uvamizi wa Israel, na pia kutoa maamuzi ya kimkakati ambayo yatafanikisha ushindi dhidi ya uvamizi na walowezi.