
Waziri mkuu wa zamani wa Uswidi na kiongozi wa Chama cha Social Democratic Eva Magdalena Andersson alisema Waziri Mkuu Ulf Kristersson amewaruhusu watu wa mrengo mkali wa kulia wenye misimamo mikali kuchochea mgogoro wa uchomaji Qur’ani Tukufu.
Alisema hayo baada ya mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari ambapo aliikosoa serikali jinsi inavyoshughulikia mzozo huo.
Mjadala wa kwanza wa viongozi wa chama baada ya mapumziko ya kiangazi ulianza na mjadala mkubwa wa kisiasa katika bunge la Uswidi siku ya Jumanne.
Anderson alikosoa alimkosoa Kristersson kwa kuhimiza siasa kali za mrengo wa kulia katika chama Sweden Democrats (SD), ambacho kinaunga mkono muungano unaoongoza wa mrengo wa kulia.
Mkimbizi wa Iraq mwenye umri wa miaka 37 aitwaye Salwan Momika amechoma nakala ya Qur’ani Tukufu marakadhaa nchini Uswidi tokea mwezi Juni mwaka huu. Vitendo hivyo vilizusha maandamano na kulaaniwa duniani kote.
Mgogoro wa kuchoma nakala za Qur’ani Tukufu umezusha maswali kuhusu mipaka ya uhuru wa kujieleza na haki ya kukera hisia za kidini.
Waziri Mkuu wa Zamani wa Usiwdi ameonya kwamba taswira ya Uswidi kama nchi isiyovumilia watu wa dini zingine ni tishio kwa uchumi na usalama wa nchi hiyo.
3485177