Hakuna furaha kwa Wakristo wa Palestina Krismasi hii huku Gaza ikishuhudia umwagaji damu
IQNA – Wakati dunia inasherehekea Krismasi, Wakristo wengi wa Kipalestina huko Beit Lahm au Bethlehem na kwingineko wanaomboleza na kuiombea Gaza, ambapo vita vya Israel vimeua kwa umati watu zaidi ya elfu 20 na kujeruhi makumi ya maelfu.