IQNA

Imam Khomeini

‘Imam; Ahadi ya Kweli ‘ Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Miaka 35 ya kuaga dunia Imam Khomeini  

21:23 - May 16, 2024
Habari ID: 3478834
IQNA – Hauli za  mwaka wa 35 tangu alipoaga dunia Imam Khomeini (RA) zitafanyika kwa kauli mbiu ya "Imam; Ahadi ya Kweli’.

Hayo yamedokezwa na kamanda wa Kikosi cha Muhammad Rasulullah  katika Mkoa wa Tehran ambaye amebainisha kuwa Imam Khomeini (RA) alitoa ahadi kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel utaangamizwa.

Jenerali Hassan Hassanzadeh amesema hayo alipotembelea kaburi la Imam Khomeini (RA) kusini mwa Tehran kwa ajili ya kumuenzi muasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Amebainisha kuwa Imam Khomeini (RA) alisema utawala wa Kizayuni wa Israel unapaswa kuangamizwa na Wapalestina warejeshewe ardhi yao na kuanzisha serikali ya Kiislamu katika ardhi hiyo takatifu.

Jenerali Hassanzadeh pia alibainisha kuwa maandalizi na uratibu wa lazima na vyombo tofauti vinavyohusiana vimefanywa kwa ajili ya kuandaa hauli ya mwaka wa 35 wa kuaga dunia Imam Khomeini (RA).

Idadi kubwa ya watu wanatarajiwa kukusanyika katika kaburi la Imam Khomeini mapema mwezi ujao ili kumuenzi marehemu muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na kutangaza upya utiifu kwa itikadi zake.

Ayatullah Ruhollah Moussavi Khomeini, anayejulikana zaidi kama Imam Khomeini, ndiye aliyeongoza Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya 1979, ambayo yalipelekea kupinduliwa Sha ambaye alitawala Iran kwa mkono wa chuma kwa uungaji mkono na Marekani.

Imam Khomeini alizaliwa mwaka wa 1902, alikua kiongozi mashuhuri wa mapambano ya taifa la Iran katika miaka ya 1970 dhidi ya utawala wa kiimla wa Shah.

Imam Khomeini alifariki tarehe 3 Juni 1989 akiwa na umri wa miaka 87 na mazishi yake ya kihistoria yalihudhuriwa na mamilioni ya wananchi wa Iran.

4215953

Habari zinazohusiana
captcha