Maandamano hayo, yaliyoandaliwa chini ya kauli mbiu "Hasira na Kuomba Usaidizi wa Mwenyezi Mungu, Kuunga Mkono Kitabu Chake, na Kutetea Matukufu ya Kiislamu ," ambapo washiriki walilaani vitendo vya kijinai vya Israel
Wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho walipiga nara za kulaani vitendo vya Wazayuni dhidi ya matukufu ya Kiislamu na wananchi wa Palestina, wakikosoa kimya na kutochukua hatua za mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.
Wamesisitiza uungaji mkono usioyumba wa Yemen kwa kadhia ya Palestina, wakiahidi kusaidia kwa kila njia licha ya changamoto zilizopo.
Waandamanaji hao wametoa wito kwa mataifa huru ya Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua madhubuti katika kutetea maeneo matakatifu na kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina, wakihimiza ulazima wa kuwa na msimamo mmoja dhidi ya utawala haramu wa Israel.
Maandamano hayo yanajiri huku picha zilizotolewa Ijumaa iliyopita zikiwaonyesha wanajeshi washenzi wa utawala haramu wa Israel wakizidharau nakala za Qur'ani Tukufu katika msikiti mmoja katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
Kituo cha habari cha Qatar cha Al Jazeera kimesema kimepata picha hizo kutoka kwenye video iliyochukuliwa na wanajeshi wa Israel ambayo ilionyesha wanajeshi wa Israel wakivamia Msikiti wa Bani Saleh ulioko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kisha kurarua na kuchoma nakala za Qur’ani Tukufu ndani ya msikiti huo.
Siku ya Ijumaa, karibu watu milioni moja walihudhuria maandamano makubwa mjini Sana'a kuelezea mshikamano wao na Wapalestina na pia kulaani kitendo cha Israel cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.
.
3489727