IQNA

Swala ya Ijumaa ya Nasr

Ayatullah Khamenei apongeza 'kazi nzuri' ya wanajeshi wa Iran katika kuishambulia Israel  

13:31 - October 04, 2024
Habari ID: 3479532
IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amepongeza "kazi nzuri ya vikosi vyetu vya jeshi" katika kutekeleza mashambulizi ya makombora dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema "ni halali na ya kisheria kabisa".

 Ayatullah Khamenei apongeza 'kazi nzuri' ya wanajeshi wa Iran katika kuishambulia Israel Ayatullah Khamenei ameyasema hayo katika hotuba ya Swala ya Ijumaa ya kila wiki ambayo imehudhuriwa na idadi kubwa ya waumini waliokusanyika katika Uwanja wa Sala wa Imam Khomeini katikati mwa Tehran.
"Kazi nzuri ya vikosi vyetu vya jeshi ilikuwa halali na ya kiesheria. Kile ambacho majeshi yetu yalichofanya ni adhabu ndogo zaidi kwa utawala ghasibu wa Kizayuni unaotenda jinai za kustaajabisha za utawala huu unaofanana na mbwa mwitu na mbwa kichaa wa Marekani," alisema.
Ayatullah Khamenei amesema, “Jukumu lolote ambalo Jamhuri ya Kiislamu inalo katika suala hili, itatekeleza kwa nguvu na ushupavu. Hatutachelewa wala hatutaharakisha kutekeleza jukumu hilo."
"Chochote chenye mantiki na busara na kwa kutegemea maoni ya watoa maamuzi ya kisiasa na kijeshi kitafanywa katika siku zijazo kama ilivyofanyika," aliongeza.
Kabla ya Swala ya Ijumaa ya Tehran kumefanyika khitma  ya kiongozi wa Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah aliyeuawa katika shambulio la kigaidi la Israel huko Beirut Ijumaa iliyopita.
Ayatullah Khamenei alimuelezea Nasrallah kama "ndugu yangu, kipenzi changu na fahari yangu, shakhsia mpendwa wa ulimwengu wa Kiislamu, na mzungumzaji mwenye ufasaha wa mataifa ya eneo, [na] kito kinachong'aa cha Lebanon".
Ayatullah Khamenei ameutaja umoja na mshikamano wa Waislamu kuwa ndio utakaowafanya wapate rehema na utukufu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ushindi dhidi ya maadui zao na akasisitiza kuwa: kwa kuzingatia kanuni za kiulinzi za Uislamu, Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu na sheria za kimataifa, kazi adhimu na ya kiustadi iliyofanywa na vikosi vya ulinzi vya Iran ya kuuadhibu utawala mnyonyaji damu wa Kizayuni ilikuwa halali kabisa na ya kisheria na Jamhuri ya Kiislamu itatekeleza kwa nguvu, umadhubuti na uwezo kamili jukumu lolote itakalohisi kuwa nalo bila kusita wala kufanya pupa.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria sera tofauti za kijeshi, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni za maadui zinazolenga kuleta migawanyiko na akasema: adui wa taifa la Iran ni adui wa mataifa ya Palestina, Lebanon, Misri, Syria, Iraq, Yemen na nchi zingine za Kiislamu na amri zote za kufanyia hujuma na kuleta mifarakano zinatolewa kwenye kituo kimoja cha maagizo; na tofauti pekee ni mbinu tu tofauti zinazotumiwa katika nchi za Kiislamu.
Ayatullah Khamenei amesisitiza kwa kusema: "Inatulazimu kufunga kwa mkanda kwa umadhubuti kwa ajili ya ulinzi, uhuru na heshima kuanzia Afghanistan hadi Yemen na kutoka Iran hadi Ghaza na Lebanon katika nchi zote za Kiislamu."
Katika khutba ya pili ya Sala ya Ijumaa aliyoisoma kwa lugha ya Kiarabu, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran aliuhutubu umma wote wa Kiislamu duniani kote na na hasahasa mataifa azizi ya Lebanon na Palestina na akasema, shakhsia halisi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, roho yake, njia na sauti yake angavu vitadumu milele.
Ayatullah Khamenei amesema, kushindwa adui muovu kuisababishia madhara makubwa taasisi imara ya Hizbullah au Hamas na Jihadul-Islami na harakati nyinginezo za Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu ndio sababu ya vitendo vyao vyake vya mauaji, uharibifu, uripuaji na mauaji ya raia na kuwaumiza kwa mateso na majonzi raia wasio na silaha na akasema: "adui anavichukulia vitendo hivi kuwa ni alama ya ushindi kwake, lakini matokeo ya mwenendo huu ni kufutwa uwepo wake wa kuaibisha katika uga wa historia".
Aidha amesisitiza kuwa: kipigo chochote kitakachotolewa dhidi ya utawala wa Kizayuni na mtu yeyote na kundi lolote ni kutoa huduma kwa eneo zima na kwa wanadamu wote.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameielezea pia njozi ya Kizayuni na Kimarekani ya kudhamini uwepo wa utawala ghasibu kuwa ni dhana potofu na haitaweza kutimia na akasema: "utawala huu bandia ni mfano wa mti muovu ambao umeweza kujikongoja kwa tabu kwa kukokotwa na Marekani, na hili nalo kwa rehma za Mwenyezi Mungu halitadumu kwa muda mrefu".
Ayatullah Khamenei amesema, genge la wahalifu la Kizayuni limeanza kufikia hatua kwa hatua hitimisho kwamba kamwe halitaweza kuzishinda Hamas na Hizbullah, na akawahutubu wananchi wanamuqawama wa Lebanon na Palestina, wapiganaji shupavu na watu wao wenye subira na ushukurivu ya kwamba: "mauaji haya ya kufa shahidi na damu hii inayomwaga chini havitadhoofisha vuguvugu lenu bali vitalifanya liwe imara zaidi".
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Muqawama wa Ghaza umeushangaza walimwengu na kuupa heshima Uislamu na akasema, operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na Muqawama wa mwaka mzima wa Ghaza na Lebanon vimeufanya utawala wa Kizayuni uingiwe na wahka na kiwewe cha kulinda uwepo wake; na akaongeza kuwa: "hii maana yake ni kwamba mapambano ya Jihadi ya wananchi wapiganaji wa Palestina na Lebanon yameweza kuurudisha miaka 70 nyuma utawala wa Kizayuni..
 
3490134

Habari zinazohusiana
captcha