IQNA

Watetezi wa Palestina

Maonyesho vibonzo vya ‘Uvimbe wa Saratani’  

21:49 - October 09, 2024
Habari ID: 3479566
IQNA - Maonyesho ya vibonzo vinavyoonyesha vipengele tofauti vya jinai za utawala wa Israel yalizinduliwa katika mji mkuu wa Uturuki wa Ankara.

Maonyesho hayo yaliyopewa anuani ya "Uvimbe wa Saratani" yanalenga utawala haramu wa Israel, na yanajumuisha kazi 40 za mchoraji vibonzo wa Iran Masoud Shojaei Tabatabaei.Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Uturuki kimefanya maonyesho hayo katika Wilaya ya Keçiören ya mji huo.
Hafla ya ufunguzi ilihudhuriwa na wanadiplomasia na wa kitamaduni kutoka Urusi, Oman, na Indonesia, wawakilishi kutoka vyama kadhaa vya kisiasa vya Uturuki, wanaharakati wa sanaa na meya wa Keçiören.
Mwambata wa Utamaduni wa Iran Seyed Qassem Nazemi amesema katika sherehe za ufunguzi kuwa maonyesho hayo ni juhudi za kuonesha ukatili na wakati huo huo udhaifu wa utawala wa Kizayuni na jinsi ulivyolidhulumu taifa la Palestina.
Alisema sanaa ni sauti ya ukweli na wasanii wanaojituma siku zote wanasimamia maadili ya kimungu na ya kibinadamu, hivyo hawawezi kubaki kutojali dhuluma na uonevu.
Vile vile amebainisha kuwa mwaka ujao umepewa jina la Mwaka wa Utamaduni wa Iran na Uturuki na kusisitiza ulazima wa kuendeleza ushirikiano wa kiutamaduni wenye kujenga kati ya nchi hizo mbili.
Shojaei Tabatabaei pia alihutubia hafla hiyo, akibainisha kuwa ameunda kazi zote zilizoonyeshwa kwenye maonyesho baada ya Operesheni ya Mafuriko ya Al-Aqsa.
Ameelezea kupinga ukatili wa utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na Palestina kuwa ni ujumbe wa kibinadamu kwa kila mtu mwenye dhamiri. .
Mzungumzaji mwingine alikuwa Meya wa Keçiören Mesut Özarslan ambaye alisisitiza haja ya kuungwa mkono kimataifa kwa upinzani wa Palestina.
Amesema ukatili wa Israel katika Ukanda wa Gaza ni jinai dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita unaozingatia sheria zote za kimataifa.
Amesisitiza azma ya manispaa ya kuunga mkono watu wa Gaza na kusema maonyesho hayo, yaliyoandaliwa kwa ushirikiano na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Uturuki, ni sehemu ya shughuli zinazolenga kuamsha dhamiri za watu kuunga mkono Gaza.

3490199
 

Habari zinazohusiana
captcha