IQNA

Mashindano ya Qur'ani Misri

Washindi watangazwa kkatika Mashindano ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Misri

15:24 - December 11, 2024
Habari ID: 3479891
IQNA - Washindi wa Mashindano ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri wametangazwa rasmi katika hafla iliyofanyika jioni ya tarehe 10 Disemba.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Wakfu za Kidini ya Misri, yalianza tarehe 7 Disemba na kuhitimishwa kwa sherehe za kutunuku baada ya Swala ya Maghrib katika Masjid Misr na Kituo cha Utamaduni katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala wa Misri.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Osama al-Azhari, Waziri wa Wakfu wa Kidini wa Misri, ambaye alitoa zawadi na kuwatambua washindi. Mashindani hayo yanawavutia washiriki kutoka kote ulimwenguni, lilishuhudia zaidi ya nchi 60 zikiwakilishwa mwaka huu. Wizara ya Wakfu hapo awali ilifichua kwamba hazina ya zawadi kwa toleo la mwaka huu imefikia rekodi ya pauni milioni 4 za Misri (takriban dola 130,000).

Zawadi hizo zilitolewa katika kategoria nyingi, huku washindani kutoka asili tofauti wakigombea kutambuliwa katika kuhifadhi, kusoma na kufasiri Qur'ani Tukufu.

3491016

captcha