IQNA

Sheikh Qais Al-KhazaliK: Kuhifadhi Hashd al-Sha’abi ni takwa la taifa la Iraq 

12:45 - September 01, 2025
Habari ID: 3481167
IQNA – Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiiraqi ya Asaib Ahl Al-Haq, Sheikh Qais Al-Khazali, amesisitiza kuwa kulinda na kuendeleza Hashd al-Sha’abi (Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi– PMU) ni takwa la watu wote wa Iraq.

Sheikh Al-Khazali amekataa fikra ya kuunganisha PMU na majeshi mengine ya Iraq, akibainisha kuwa wazo hilo lilianzia kwa balozi wa Uingereza.

Akizungumzia unafiki wa mataifa ya Magharibi, alisema: “Tunapodai kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani, wao husema bado kuna Daesh (ISIL/ISIS). Lakini wao wanapodai kuvunjwa kwa PMU, husema Daesh imedhoofika na hakuna haja tena ya Hashd al-Sha’abi.”

Al-Khazali alieleza kuwa kuwepo kwa PMU kumeipa Iraq nguvu ya ziada, na kikosi hiki kimekuwa chanzo cha kujiamini kwa kweli na njia ya kudumisha mshikamano wa kitaifa.

“Tulifanikiwa kupata ushindi wa kweli kwa rasilimali zetu wenyewe, kwa fatwa ya Marja’iyya, kwa jitihada za makundi ya muqawama (mapambano), kwa juhudi za wana wa taifa hili, na kwa msaada wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Hizbullah ya Lebanon.”

Sheikh huyo alisema kuwa Daesh lilikuwa tishio kubwa na gumu zaidi kwa Iraq, na lengo lake lilikuwa kuchochea vita vya kidini kote nchini humo.

Hashd al-Sha’abi ni taasisi ya kiserikali inayoundwa na takribani makundi 40 ya wapiganaji wa kujitolea kupambana na ugaidi, yakiwemo makundi ya Ki-Shia kama Asa’ib, pamoja na ndugu zao Waislamu wa Kisunni, Wakristo na Wakurd.

Kikosi hiki ni sehemu ya majeshi rasmi ya Iraq na hufanya kazi chini ya amri ya Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Iraq.

PMU iliundwa  baada ya kutolewa kwa fatwa tukufu na Marja’ mkubwa, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Sistani (hafidhahullah), akibainisha wajibu wa Jihad dhidi ya Daesh.

/349443

captcha