IQNA

18:11 - August 17, 2026
Habari ID: 3482638

Wizara ya Awqaf ya Palestina yaandaa Mashindano ya 25 ya Qur’an ya Al-Aqsa

IQNA – Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kidini ya Palestina imetangaza kuwa Mashindano ya 25 ya Kuhifadhi na Tafsiri ya Qur’an ya Al-Aqsa yatafanyika kwa ushiriki wa wanaharakati wa Qur’an kutoka maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza.

pa

Wizara hiyo ilitangaza kumalizika kwa mchakato wa usajili kwa ajili ya toleo la 25 la mashindano hayo baada ya kukamilisha uingizaji wa taarifa za washiriki 1,863, wanaume na wanawake, kwa mujibu wa tovuti ya Al-Rai.

Hatua hii imefikiwa baada ya usajili wa washiriki 1,863, ili kujiandaa kwa hatua ya awali, ambayo imepangwa kuanza leo, Jumapili, chini ya usimamizi wa kamati ndogo maalum.

Kulingana na takwimu za mwisho za usajili wa kielektroniki, wizara iliripoti kiwango kikubwa cha ushiriki katika mashindano hayo, ikitangaza kuwa washiriki 622 wanaume na 1,241 wanawake wamejiandikisha kwa ajili ya hafla hiyo.

Katika kitengo cha kwanza, kuhifadhi Qur’an nzima, kuna washiriki 261; katika kitengo cha pili, kuhifadhi Juzuu 20, kuna washiriki 185; na katika kitengo cha tatu, kuhifadhi Juzuu 10, kuna washiriki 1,417, huku kitengo cha tatu kikiwa na kiwango cha juu zaidi cha ushiriki.

Kwa mujibu wa ratiba iliyoidhinishwa, hatua za awali zitaanza katika makao makuu ya kamati ndogo zinazosimamia mashindano hayo.

Wizara ilieleza kuwa toleo la 25 limeandaliwa kwa michango ya ukarimu kutoka kwa wafadhili wa Omani na kwa uungaji mkono na udhamini wa kampeni ya misaada ya dharura ya Madad al-Khair.

Wizara ilisisitiza kuwa ushiriki huu mpana unaakisi uwepo wa kina wa Qur’an katika jamii ya Palestina na hamu ya watu wa Ukanda wa Gaza ya kutaka kujifunza Kitabu cha Mwenyezi Mungu kupitia kuhifadhi na kutafakari aya zake, licha ya hali ngumu na ya kipekee inayolikabili eneo hilo kufuatia mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala dhalimu wa Israel.

Wizara ilitoa shukrani kwa washiriki wote, familia zao, na walimu wa Qur’an, na kuwatakia kila la heri washiriki wote katika hatua za awali na raundi zinazofuata za mashindano.

4370044

Habari zinazohusiana
captcha