IQNA

16:13 - August 18, 2026
Habari ID: 3482645

Pogba, nyota wa soka wa Ufaransa aonyesha mshikamano na Gaza

IQNA – Paul Pogba, nyota wa soka wa Ufaransa, ameonyesha mshikamano na Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, wanaokabiliwa na mauaj ya kimbari ya Israel, kwa kuposti picha ya mtoto wa Kipalestina akiwa miongoni mwa vifusi na uharibifu wa Gaza kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram.

a

“Ninawezaje kuwa na huzuni (kuhusu matatizo yangu binafsi) wakati ninapoona haya?” Pogba aliandika kando ya picha hiyo, kama ilivyoripotiwa na Kituo cha Habari cha Palestina.

Katika ujumbe huu, alibainisha udogo wa matatizo yake ya kimichezo ikilinganishwa na mateso makubwa yanayosababishwa na mauaji ya kimbari yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza.

Msimamo huu umechukuliwa wakati Pogba mwenyewe akikabiliwa na sintofahamu kuhusu mustakabali wake wa kimichezo, huku uongozi wa klabu ya Ufaransa ya Monaco ukianza mazungumzo ya kusitisha mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote kufuatia majeraha yake ya mara kwa mara na kupungua kwa ushiriki wake katika mechi.

3498691

Habari zinazohusiana
captcha