IQNA

13:30 - August 19, 2026
Habari ID: 3482650

Wairani waadhimisha Siku ya Arubaini tangu Mazishi ya Kiongozi Shahidi

IQNA – Hafla ya Khitma kwa ajili ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ilifanyika mjini Tehran Jumanne jioni, ikiwa ni siku ya arubaini tangu kuzikwa kwake.

Hafla hiyo haikuwa tu Khitma kwa ajili ya Kiongozi Shahidi. Badala yake, wananchi walihudhuria kwa wingi ili kutangaza upya ahadi yao ya kuendeleza njia ya shahidi huyo, kulinda misingi na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu, na kusimama katika njia ambayo alijitolea maisha yake kwa ajili yake.

Hafla hiyo iliandaliwa na Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ikiwa na kaulimbiu: “Tuko katika ahadi na wewe hadi mapambazuko ya Siku ya Kiyama.”

Idadi kubwa ya wananchi pamoja na maafisa waandamizi wa serikali na jeshi walihudhuria kumbukumbu hiyo, iliyoanza saa 11:00 jioni katika eneo la Musalla wa Imam Khomeini (RA) mjini Tehran. Hafla hiyo ilianza kwa kisomo cha Qur’ani Tukufu kilichosomwa na Qari Younes Shahmoradi.

Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa Rais Masoud Pezeshkian, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu Mohammad Bagher Ghalibaf, Mkuu wa Idara ya Mahakama Hojjat al-Islam Gholam-Hossein Mohseni Ejei, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Brigedia Jenerali Esmail Qaani, pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais Mohammad Reza Aref.

Baada ya kisomo cha Qur’ani, munshid Morteza Taheri aliwasilisha tenzi na maombolezo ya kumuenzi shahidi huyo.

Bendera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zilionekana zikipepea katikati ya umati. Kando yake, ilionekana pia bendera nyekundu yenye kaulimbiu “Ya Litharat al-Husayn”, ambayo hutazamwa kama ishara ya kulipiza kisasi kwa damu ya Kiongozi Shahidi.

Picha za Kiongozi Shahidi pia zilikuwa zilisambaa katika hafla hiyo. Wananchi walizinyanyua picha hizo juu ya mikono yao, jambo lililokumbusha kwamba njia yake haikukomea kwa kuuawa kwake shahidi, bali inaendelea kupitia wananchi.

Hafla hiyo iliendelea kwa kisomo kingine cha aya za Qur’ani Tukufu kilichotolewa na Qari Ahmadi-Vafa.

Iranians’ New Pledge on 40th Day after Martyred Leader’s Funeral

Hafla kama hiyo inatarajiwa kufanyika Jumatano katika mji wa Qom, baada ya Swala ya Magharibi na Isha, kwenye Haram Tukufu ya Hadhrat Ma’sumah (SA).

Hafla nyingine itafanyika Alhamisi, inayosadifiana na usiku wa kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Hasan al-Askari (AS), baada ya Swala ya Magharibi na Isha, katika mji mtakatifu wa Mashhad.

4370471

captcha