IQNA

17:07 - August 22, 2026
Habari ID: 3482657

Aliyevunjia heshima Uislamu nchiniMalaysia afungwa jela nchini

IQNA – Mahakama moja katika jimbo la Johor, Malaysia, imemhukumu mwanamume kifungo cha jela kwa kuidhalilisha na kuivunjia heshima dini ya Kiislamu

m

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 56, raia wa Singapore, alihukumiwa kifungo cha siku 14 jela na kutozwa faini ya ringgit za Malaysia 7,000 (dola za Marekani 1,733) na mahakama ya Johor siku ya Ijumaa, Agosti 21, baada ya kukiri kuwa na hatia ya kuitukana dini ya Kiislamu wakati wa ziara yake katika jimbo hilo la Malaysia.

Mohamed Anim Atam, ambaye ni mlinzi kutoka Singapore na hakuwakilishwa na wakili, alihukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Johor Bahru, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Malaysia.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Mohamed Anim alitamka kwa makusudi maneno ya kuidhalilisha dini ya Kiislamu, akiwa na nia ya kujeruhi hisia za kidini za mtu mwingine, kosa linalotajwa chini ya Kifungu cha 298 cha Sheria ya Adhabu, liliripoti gazeti la The Star.

Mohamed Anim alidaiwa kutenda kosa hilo tarehe 30 Julai, akiwa safarini katika gari la usafiri linaloombwa kupitia programu ya simu, kutoka Jalan Tun Razak kuelekea Jalan Meldrum.

Hakimu A. Shaarmini aliamuru kifungo hicho kianze kuhesabiwa kuanzia siku aliyokamatwa, Jumanne; la sivyo, angekabiliwa na kifungo cha ziada cha miezi mitatu jela.

Kosa hilo linaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha juu cha mwaka mmoja jela, faini, au adhabu zote mbili.

Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti kuwa, kwa mujibu wa maelezo ya kesi hiyo, Mohamed Anim alidai wakati wa safari hiyo kwamba  eti Qur’ani haina huruma na eti inajikita katika mauaji pekee.

Matamshi hayo yalisikika na dereva wa gari hilo la usafiri, Muhamad Danial Haikal Nadzahakim, ambaye baadaye alisambaza kwenye mitandao ya kijamii video ya mazungumzo hayo iliyodumu kwa dakika mbili. Video hiyo ilisambaa kwa kasi.

Ripoti ya polisi iliwasilishwa tarehe 31 Julai. Mohamed Anim alikamatwa baadaye tarehe 18 Agosti katika Jengo la Sultan Iskandar, kando ya Jalan Lingkaran Dalam, eneo la Bukit Chagar.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo siku ya Ijumaa, aliomba apewe faini badala ya kifungo, akitaja kuwa ana shinikizo la juu la damu na yuko katika mchakato wa talaka unaoendelea, ambao unamtaka kufika mbele ya Mahakama ya Sharia nchini Singapore, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari.

Naibu Mwendesha Mashtaka wa Umma, Eizlan Azhar, aliomba mahakama itoe adhabu inayolingana na uzito wa kosa hilo. Alisema kosa hilo limegusa masuala nyeti sana nchini Malaysia yanayohusu kabila, dini na ufalme, na limezua malalamiko makubwa ya umma kwenye mitandao ya kijamii, liliripoti gazeti la Malay Mail.

3498736

Habari zinazohusiana
captcha