IQNA

17:15 - August 22, 2026
Habari ID: 3482660

Washindi wa Mashindano ya Qur’ani ya Makka Watunukiwa

IQNA – Washindi wa toleo la 46 la Mashindano ya Kimataifa ya Mfalme Abdulaziz ya Kuhifadhi, Kusoma, na kufasiri Qur’ani Tukufu wametunukiwa katika hafla iliyofanyika ndani ya Msikiti Mtukufu (Masjid al-Haram) huko Makka.

Hafla hiyo ilifanyika chini ya udhamini na kwa niaba ya Mfalme wa Saudi Arabia, ikiongozwa na Naibu Gavana wa Mkoa wa Makka, Mwanamfalme Saud bin Mishaal bin Abdulaziz.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu, Da’wah na Mwongozo wa Saudi Arabia, Sheikh Dkt. Abdullatif Al Alsheikh, alisisitiza kuwa mashindano haya ni ushahidi wa kujitolea katika kuitumikia Qur’ani Tukufu, kuwaunga mkono wahifadhi wake, na kuwaleta watu pamoja kupitia mwongozo na uadilifu.

Alibainisha ongezeko la idadi ya washindi kutoka 12 hadi 50, sambamba na kupanda kwa jumla ya zawadi za fedha kutoka Riyali milioni 1.1 hadi zaidi ya Riyali milioni 10.

Katika kuhitimisha sherehe hiyo, Mwanamfalme Saud bin Mishaal bin Abdulaziz aliwatuza washindi pamoja na wajumbe wa jopo la majaji waliosimamia mashindano hayo.

3498726

captcha