IQNA – Mwanaharakati wa mrengo mkali wa kulia nchini Marekani, ambaye amekuwa akifanya vitendo vya kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu mara kadhaa, amekamatwa jijini Minneapolis.
Polisi wa Minneapolis wamemkamata Jake Lang pamoja na wafuasi wake sita baada ya kuwepo kwa machafuko siku ya Jumamosi nje ya jengo la serikali ya mji huo.
Polisi wamesema kuwa Lang na kikundi chake walielekeza gari lao kwenye njia ya watembea kwa miguu mbele ya jengo la serikali kuelekea kwenye mkusanyiko wa watu. Video za mitandao ya kijamii zilionyesha Lang akiwa amesimama juu ya gari la aina ya pickup akiwa ameshikilia bango lenye maneno ya ubaguzi wa rangi.
Video hizo pia zilionyesha Lang na wanaharakati wenzake wakipambana na waandamanaji wa upande wa pili. Polisi wa Minneapolis hatimaye walitokeza nje ya jengo la serikali, huku Lang akiondoka kwa gari wakati huo huo.
Mkuu wa polisi wa muda, Bill Petersen, alieleza katika mkutano na wanahabari kuwa “kemikali inayowasha (inayodhaniwa kuwa ni mace) ilitumiwa na pande zote mbili.” Petersen alisisitiza kuwa “hakuna ushahidi” wowote unaothibitisha kuwa polisi walitumia kemikali hizo.
Polisi walisema walifuatilia magari mawili yaliyokuwa na Lang. Moja lililozuiwa karibu na barabara ya Washington Avenue na Interstate 35W, huku jingine likipatikana karibu na Mall of America.
Kila mtu aliyekuwa ndani ya magari hayo mawili alikamatwa kwa tuhuma za kusababisha machafuko. Lang alifikishwa katika gereza la Hennepin County bila ruhusa ya kutoa dhamana. Polisi hawajajibu ombi la kupata majina ya wafuasi wake sita waliokamatwa pia.
Meya Jacob Frey amesema kuwa polisi bado wanokusanya ushahidi, na uchunguzi dhidi ya Lang na wafuasi wake unaendelea.
“Hakika, kuna uwezekano wa mashtaka mengine, lakini bado tunahitaji ushahidi ili kubainisha kilichotokea. Tuko katika hatua za awali za uchunguzi wa ziada kwa sasa,” alisema Frey.
Petersen alieleza kuwa maafisa watatu waliumia, huku mmoja akipelekwa hospitalini na kisha kutolewa. Mmoja wa maafisa hao huenda alikanyagwa mguu na moja ya magari yaliyokuwa yakiondoka, na mwingine alipigwa na kitu kilichotupwa. Aliongeza kuwa wachunguzi wamepokea ripoti ya mtu aliyeshambuliwa na wanajaribu kupata maelezo kutoka kwa mwathiriwa huyo.
Lang alikuwa mjini humo akiendesha mkutano kwa ajili ya Shiloh Hendrix, mwanamke kutoka Rochester ambaye mnamo mwaka 2025 alimtukana mtoto wa kiume wa miaka 8 mwenye ulemavu wa kiakili (autism) kwa kutumia maneno ya ubaguzi wa rangi akiwa uwanjani. Hendrix hakuonekana na hatia ya kosa la kuvuruga utul. Hendrix hakuonekana na hatia ya kosa la kuvuruga utulivu na hatia mnamo Julai kwa kosa lile lile alipomfanyia mtu mwingine aliyekuwa akirekodi tukio hilo.
Wengine wanne ambao hawakuwa na uhusiano na Lang pia walikamatwa, akiwemo mmoja kwa kosa la machafuko na mwingine kwa kosa la kushambulia, alisema Petersen.
3498753