IQNA

20:22 - August 30, 2026
Habari ID: 3482695

Msomi wa Lebanon apongeza Iran kwa kutetea Palestina

IQNA – Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imebaki kuwa mwaminifu kwa watu wa Palestina na mapambano yao, huku ikijitahidi kwa dhati kwa ajili ya ukombozi wa al-Quds, kulingana na msomi wa Lebanon, Sheikh Zuhair Othman Jaeed, ambaye ni Mratibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Amal ya Lebanon.

Zuhair Othman Jaeed

Katika mahojiano na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) pembezoni mwa Kongamano la 40 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu mjini Tehran, Sheikh Jaeed alisisitiza kuwa Iran imechukua mzigo mzito wa vita na vikwazo kwa ajili ya kufanikisha umoja wa Umma wa Kiislamu.

Kuhusu Umoja wa Kiislamu na Katazo la Kutukana Matukufu: Sheikh Jaeed alibainisha kuwa Kiongozi Shahidi wa Ummah, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, alikuwa mstari wa mbele zaidi kuliko mamlaka nyingi za kidini za Kishia katika kusisitiza katazo la kutovunjia heshima matukufu ya jamii ya Kisunni, ikiwa ni pamoja na masahaba na wake za Mtume (SAW). "Alitoa agizo kwa serikali na taasisi za kiserikali likitangaza kuwa matusi yoyote dhidi ya watu watukufu katika madhehebu zingine za Kiislamu. Aidha alisisitiza kuhusu Umoja wa Kiislamu na umuhimu wa kadhia ya Palestina. “Kwa upande wetu sisi Masunni, ni fahari na heshima kubwa kuona kuwa Ayatullah Khamenei hakuchukulia suala la Umoja wa Kiislamu kama nadharia ya kwenye vitabu pekee. Badala yake, aliliona kama agizo linalotokana na misingi ya imani na utiifu kwa Mwenyezi Mungu, na akafanya kazi ya kulitekeleza kwa vitendo, si kwa maneno tu au nadharia tupu.”

IQNA – Je, unatafsiri vipi nafasi ya kadhia ya Palestina, al-Quds, na mhimili wa Muqawama (mapambano) katika fikra za Kiongozi huyo aliyetangulia mbele ya haki?

Sheikh Jaeed: “Imam Khamenei ni mwanafunzi mahiri wa shule ya fikra ya Imam Khomeini (RA). Hivyo, kwetu sisi katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, tangu Mapinduzi haya yalipoanza na kushinda, dira kuu ya mfumo huu imejikita kwenye mambo mawili muhimu na ya lazima. Pamoja na kwamba kuna masuala mengine ambayo bila shaka ni muhimu kwa taifa la Iran, kwetu sisi, kile kilichokuwa na uzito ni Umoja wa Kiislamu na kadhia ya Palestina. Jamhuri ya Kiislamu imebaki kuwa mwaminifu kwa watu wa Palestina na mapambano yao. Imejitolea kwa dhati kuikomboa Palestina na kuwaunga mkono wananchi wake katika kudai haki zao; na kiukweli, Jamhuri ya Kiislamu imelipa gharama nzito sana kwa kushikilia msimamo huu.”

 IQNA – Qur’ani Tukufu ina mtazamo gani kuhusu dhana ya umoja na ni njia ipi ya kuufikia?

Sheikh Jaeed: “Qur’ani Tukufu imetoa amri ya wazi na ya kiungu kwamba Waislamu lazima wawe wamoja. Mwenyezi Mungu anasema: ‘Hakika huu ni Ummah wenu, Ummah mmoja, na Mimi ni Mola wenu, basi niabuduni Mimi’ (Surah Al-Anbiya: 92). Na katika aya nyingine inasema: ‘Hakika dini mbele ya Allah ni Uislamu.’ (Surah Al-Imran: 19). Uislamu ni mmoja. Ndani ya Uislamu, hakuna dini inayoitwa ‘Shia’ wala dini inayoitwa ‘Sunni.’ Uislamu ni dini moja; hizi ni njia tofauti tu za ibada. Kwa hivyo, Uislamu ni dini ya kuungana na umoja. Qur’ani inatuamuru umoja na kusema: ‘Na shikilieni kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.’”

 3498832

Habari zinazohusiana
captcha