IQNA

20:31 - August 30, 2026
Habari ID: 3482696

Kiongozi Shahidi alikuwa mbeba bendera ya umoja wa Kiislamu kupitia mtazamo wa Qur’ani

IQNA – Msomi mashuhuri wa Lebanon amesisitiza kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, alikuwa na mtazamo wa kina na wa kipekee kuhusu umoja wa Kiislamu.

Sayed Ali Fadlallah

Katika mahojiano na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) pembezoni mwa Kongamano la 40 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu, Seyed Ali Fadlallah alieleza kuwa Kiongozi huyo aliamini, kwa mtazamo wa Qur’ani, kuwa juhudi za kufikia umoja wa Waislamu ni wajibu wa kila mmoja na jukumu la pamoja la Ummah.

Seyed Fadlallah alibainisha kuwa Kiongozi Shahidi hakuchukulia umoja kama mkakati wa muda mfupi wa kisiasa tu; badala yake, aliamini kuwa haiwezekani kufikia umoja wa kweli bila kuzingatia amri za Qur’ani. “Aliamini kuwa silaha inayoweza kutumika dhidi ya umoja wa Kiislamu ni matusi dhidi ya matukufu na ishara za madhehebu mbalimbali, na fatwa yake ilisisitiza kuwa ni haramu kabisa kuvunja heshima ya alama na matukufu ya madhehebu ya Kiislamu,” alisisitiza.

Msomi huyo wa Lebanon aliongeza kuwa wakati mwingine mtu anaweza kuwa anatafuta haki au upendeleo wake, lakini kwa kutojitambia, anaweza kuwakosea wengine katika mchakato huo. Hivyo, ni muhimu kuwa mwangalifu ili usivunje heshima ya imani na misingi ya wengine, iwe kwa makusudi au kwa kutokutenda kwa umakini.

Aliyekuwa kiongozi wa sala za Ijumaa jijini Beirut alieleza kuwa umoja wa Kiislamu ni silaha thabiti ya kukabiliana na aina yoyote ya fitna (fitina) na wale wanaotafuta kuleta machafuko. Alionya kuwa yeyote anayetafuta utengano na fitina atakuwa akipambana dhidi ya silaha hii muhimu.

Aidha, Sayed Ali Fadlallah alisisitiza kuwa baadhi ya fatwa zinazotolewa na watu wasio na elimu ya kina zinaweza kufanya juhudi za kuleta umoja kushindwa, na hivyo kuruhusu fitina itumike kama chombo cha kuleta machafuko.

Alimalizia kwa kuorodhesha vikwazo vikubwa vya ndani na nje vinavyozuia umoja, akisema kuwa moja ya vikwazo hivyo ni hisia miongoni mwa wafuasi wa madhehebu mbalimbali kwamba, wakijumuika na madhehebu mengine, watadhoofisha au kuwavunja heshima viongozi na alama zao.

“Hivyo basi, ili kuondoa mtazamo huo, ni lazima kusisitizwa mara kwa mara kwamba umoja wa Kiislamu haumaanishi kuacha dini au kusahau misingi na alama za kidini; bali unamaanisha umoja katika misingi na imani zinazofanana,” alihitimisha.

3498835

Habari zinazohusiana
captcha