IQNA

20:37 - August 30, 2026
Habari ID: 3482697

Rais wa Iran: Mtume Muhammad (SAW) ni mbeba ujumbe wa amani kwa watu wote ulimwenguni

IQNA – Akitoa pongezi kwa mataifa ya Kiislamu kwa mnasaba wa maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu amekuwa daima mbeba ujumbe wa amani na usalama kwa wanadamu wote ulimwenguni.

r

Katika ujumbe wake maalum alioutuma jioni ya Jumamosi kuamkia maadhimisho hayo, ulioelekezwa kwa viongozi na wananchi wa nchi za Kiislamu, Rais Pezeshkian alisisitiza kuwa Waislamu kote duniani wanapaswa kutegemea misingi ya imani na azma yao ya pamoja ili kuimarisha umoja wao na kupaaza hadhi ya Uislamu kote ulimwenguni.

“Natumai kwamba kwa baraka na neema za masiku haya matukufu… tutakuwa amana na wajumbe wanaosimamia kuleta usalama, uadilifu, na maridhiano katika ulimwengu mzima, na hususan katika nchi za Kiislamu,” alisema Pezeshkian katika ujumbe huo.

Alibainisha kuwa Mtume Muhammad (SAW) daima amekuwa nguzo ya amani na utulivu kwa watu wote, akimwelezea kama Mtume ambaye jina la dini yake linamaanisha amani na ambaye lakabu yake kuu ni ‘Rehema kwa Walimwengu’ (Rahmatan lil-'Alamin).

Rais wa Iran aliongeza kuwa mwenendo na maisha ya Mtume Muhammad (SAW), yanayotambulika kama Seerah, yanapaswa kuwa “kielelezo cha juu kabisa cha ukamilifu na mfano halisi wa maadili mema na fadhila adhimu za kiutu.”

“Seerah ya Mtume huyu mtukufu imekuwa daima taa yenye kung’aa inayomulika na kuongoza njia ya mwanadamu katika dhoruba na changamoto za ulimwengu huu,” alihitimisha Rais Pezeshkian.

3498838

Habari zinazohusiana
captcha