IQNA – Nakala adhimu ya Qur’ani inaonyeshwa katika Makumbusho ya Qur’ani Tukufu yaliyopo katika Eneo la Utamaduni la Hira mjini Makka, ikionyesha mbinu za awali za uandishi wa Qur’ani.
Nakala hiyo ni ukurasa mmoja kutoka katika Qur’ani inayokadiria kuwa imetoka karne ya tatu ya Hijri, ambapo inaendana na karne ya tisa ya Miladia (CE). Hii ni hazina ya kihistoria inayonyesha hatua za awali za utengenezaji wa maandishi ya Qur’ani.
Nakala hiyo ya Msahafu inayoonyeshwa inajumuisha sehemu ya Surah Maryam, iliyoandikwa kwenye ngozi (parchment) kwa kutumia wino mwekundu.
Maandishi hayo hayana alama za sauti wala nukta za utambulisho wa herufi , jambo ambalo ni sifa kuu ya hatua za awali za uandishi wa maandishi ya Qur’ani.
Onyesho hili linatoa fursa kwa watazamaji wa makumbusho kujifunza kuhusu mageuzi ya uandishi wa Qur’ani na mbinu zilizotumiwa kurekodi Qur’ani katika karne za kwanza za Kiislamu.
Makumbusho ya Qur’ani Tukufu ni miongoni mwa vituo vikuu katika Eneo la Utamaduni la Hira, likitoa uzoefu wa kielimu na wa kijamii unaosisitiza historia ya Qur’ani, mageuzi ya uandishi wa nakala za Qur’ani, na aina mbalimbali za ulinzi na utunzaji ulioonyeshwa kwake katika nyakati zote.
3498842