IQNA – “Chuo cha Kitaalamu cha Hija” kimepangwa kuzinduliwa nchini Iran ili kuboresha uwezo wa kitaalamu na kiufundi wa wanazuoni wanaoongoza misafara ya Hajj, afisa mmoja amesema.
Hojjat-ul-Islam Akhavian, Mkurugenzi wa Elimu na Utamaduni katika Ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi katika Masuala ya Hija na Ziara, alisema chuo kiku inalenga kuimarisha uwezo wa kitaalamu na kiufundi wa wanazuoni wa misafara hiyo na kuongeza utayari wao wa kujibu mahitaji na maswali mbalimbali ya mahujaji.
Akirejelea tofauti katika mahitaji na maswali ya mahujaji, alisema, “Kwa kuzingatia kuwa mahujaji wana hali na mahitaji tofauti, wanazuoni wanaoongoza misafara ya Hajj lazima wawe na uwezo wa kisayansi, kitaalamu, na kiufundi unaohitajika ili kujibu masuala ya sasa.”
Kwa hivyo, aliongeza, mwaka huu, kwa mara ya kwanza, Chuo cha Kitaalamu cha Hija kitaundwa kwa ajili ya wanazuoni watakaotumwa kwa ajili ya Hija kila mwaka, na mojawapo ya programu zake kuu ni kufanya mikutano maalum katika uwanja wa masuala yanayohusiana na yanayohitajika kwa ajili ya ibada za Hija.
Katika mikutano hii, Hojjat-ul-Islam Akhavian alisema, wataalamu wanawasilisha mada zinazohusiana na masuala ya ibada katika mfumo wa warsha, na wanazuoni, kwa kushiriki kikamilifu katika mikutano hii, huimarisha ujuzi wao, na kufahamiana na masuala ya kivitendo na mahitaji ya mahujaji.
Wanazuoni hao pia watafanyiwa mahojiano ya kisayansi ili waweze kuondoka kuelekea ardhi ya Wahyi (Hijaz) wakiwa na maandalizi kamili ya kitaalamu katika uwanja wa masuala ya ibada ya Hija, alisema.
4373675
Zenye maoni mengi zaidi