IQNA

16:08 - September 05, 2026
Habari ID: 3482721

Soka Palestina yarejea baada ya miaka 3 ya mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa na Israel

IQNA – Soka huko Palestina imeanza tena siku ya Ijumaa kupitia mashindano ya klabu katika Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Gaza, na kambi za wakimbizi nchini Lebanoni, baada ya kusimamishwa kwa karibu miaka mitatu kutokana na vita vya kigaidi vya mauaji ya kimbari vinavyofanywa na Israel.

s

Shirikisho la Soka la Palestina limeandaa mashindano hayo ya “Kombe la Maelfu ya Mashahidi”, ambapo mechi za ufunguzi zilifanyika kwa wakati mmoja katika maeneo hayo matatu, ikiwemo Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Gaza, na kambi za wakimbizi nchini Lebanoni.

Klabu takribani 244 kutoka Ukingo wa Magharibi, Gaza, na jamii ya watu waliotawanyika (diaspora), zinashiriki katika mashindano hayo.

Uchaguzi wa makundi ulifanyika kwa wakati mmoja katika matawi mbalimbali ya chama hicho mnamo Septemba 1.

Shirikisho hilo limeyapa mashindano hayo jina hilo kwa kumbukumbu ya wanariadha wa Palestina ambao wameuawa shahidi  na Israel wakati wa vita vyake dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Mustafa Siyam, Katibu Mkuu wa Chama cha Vyombo vya Habari vya Michezo ya Palestina, alisema mashindano haya yanaashiria kurejea kwa shughuli za michezo baada ya zaidi ya msimu mitatu za kusimamishwa.

Alisema kuwa vita hivyo pia viliwalenga wanariadha wa Palestina na miundombinu ya michezo, huku zaidi ya wanariadha 1,000, wakiwemo wachezaji, makocha, na waamuzi, wakiuawa.

Mashindano hayo yalipewa jina la mashahidi wa harakati za michezo, ili kuenzi uaminifu na dhabihu zao, alisema Siyam. Uzinduzi wake unawakilisha “ujumbe kwamba maisha ya michezo yanarejea kama kawaida.”

Kurejea kwa mechi katika Gaza kuna umuhimu wa kipekee kutokana na hasara kubwa ya kibinadamu na mali iliyofanywa dhidi ya michezo ya Palestina tangu Israel ilipoanzisha vita vyake dhidi ya eneo hilo mnamo Oktoba 2023.

Katika Ukingo wa Magharibi, mashindano hayo pia yanafuatia kusimamishwa kwa mashindano ya ndani kwa msimu mitatu kutokana na kuongezeka kwa ukali wa vitendo vya Israel, jambo ambalo limezuia uwezo wa klabu na wachezaji kufanya mazoezi, kusafiri, na kuandaa mechi kwa kawaida.

3498901

Habari zinazohusiana
captcha