IQNA

11:26 - September 06, 2026
Habari ID: 3482725

Mkutano wa Cairo wajadili ‘Mtume wa Rehema katika Kioo cha Ushairi wa Kiajemi’

IQNA – Kikao kilichoitwa “Mtume wa Rehema (SAW) katika Kioo cha Ushairi wa Kiajemi na Muziki” kimefanyika mjini Cairo, mji mkuu wa Misri.

cairo

Kikao hicho kilihudhuriwa na kikundi cha maprofesa vijana wa lugha na fasihi ya Kiajemi kutoka vyuo vikuu vya Misri. Katika mazingira ya mwingiliano hai, washiriki walichunguza mifumo ya kujitolea na upendo kwa Mtume Muhammad (SAW) katika ushairi, muziki, na mila za kitamaduni za Iran na Misri.

Katika sehemu ya kwanza ya kikao hiki, kilichofanyika kwa juhudi za Kituo cha Kitamaduni cha Iran nchini Misri, washiriki walichagua beti za washairi wa Kiajemi zinazomsifu Mtume Muhammad (SAW) na kuzisoma kwa hadhira.

Baada ya kila usomaji, kulikuwa na mjadala kuhusu jinsi utu wa Mtume (SAW) unavyojitokeza katika ushairi huo, dhana na maudhui yaliyotumika, pamoja na sababu za kuchagua shairi husika.

Sehemu hii, huku ikitoa fursa ya kufanya mazoezi ya usomaji na mazungumzo kwa lugha ya Kiajemi, imeweka msingi wa uzingatiaji mkubwa zaidi wa uchangamano wa kifasihi na kimaana wa ushairi wa Kiajemi.

Kisha, klipu ya usomaji wa mashairi ya Rumi ya Kiajemi katika kumsifu Mtume Muhammad (SAW) ilichezwa, na muziki wa shairi hilo, taswira za kishairi, pamoja na namna ya kueleza mapenzi na kujitolea kwa Mtume (SAW) vilikuwa miongoni mwa mada za mjadala baada ya kuonyeshwa kwa kazi hiyo.

Sehemu nyingine ya mpango huo iliwekwa kwa ajili ya kuonyesha filamu fupi ya hali halisi kuhusu tambiko la “Ngoma Elfu” katika maeneo ya Wakurdi wa Iran, ambapo kikundi cha watu hucheza ngoma kwa pamoja katika hafla mbalimbali za kitamaduni na kidini, zikiwemo sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad (SAW).

Kwa kulinganisha mifano iliyowasilishwa kutoka utamaduni wa Iran na uzoefu wa kitamaduni wa Misri, washiriki walibadilishana mawazo kuhusu nafusu nafasi ya ushairi, muziki, kasida, za pamoja katika kumtukuza Mtume Tukufu (SAW) katika jamii hizo mbili.

3498912

captcha