IQNA – Maandamano ya kuunga mkono Palestina yamefanyika katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, siku ya Jumamosi.
Waandamanaji wanaounga mkono Palestina walikusanyika katika Uwanja wa Chatelet kufuatia wito wa Chama cha EuroPalestine, kabla ya kuandamana kuelekea Place de la Bourse.
Wakiwa wamebeba bendera za Palestina na mabango yaliyoandikwa “Susieni Israel” (Boycott Israel) na “Uhuru kwa Wapalestina,” waandamanaji waliiomba serikali ya Ufaransa kuiwekea Israel vikwazo.
Waandamanaji walipiga nara za kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza na kueleza azma yao imara ya kuendelea kupaza sauti zao dhidi ya dhuluma hizi.
Washiriki pia walibeba picha zinazoonyesha maangamizi ya kimbari huko Gaza sambamba na picha za Holocaust wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, kama njia ya kuonyesha ukinzani wa kimaadili wa jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni.
Pia walipinga vikali ubomoaji wa nyumba za Wapalestina unaofanywa na Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, na jitihada za utawala huo za kuwafurusha kwa nguvu Wapalestina kutoka katika ardhi yao ya asili.
3498918
Zenye maoni mengi zaidi