IQNA

14:47 - September 07, 2026
Habari ID: 3482732

Mchochezi wa mrengo wa kulia nchini Marekani, Jake Lang, avunjia heshima Qur’an Tukufu tena

IQNA – Jake Lang, mwanaharakati wa siasa za mrengo wa kulia nchini Marekani na mfuasi wa Rais Donald Trump, amefanya kitendo cha kuchukiza cha kuvunjia heshima Qur’an Tukufu, ikiwa ni mwendelezo wa vitendo vyake vya chuki dhidi ya Uislamu.

Jake Lang

Katika kitendo cha wazi cha uchochezi huko New York, Lang alirarua nakala ya Qur’an Tukufu. Kwa mujibu wa picha na ripoti zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, tukio hilo lilitokea mara baada ya Lang kuhutubia katika kanisa la ATLAH Ministries, linaloongozwa na Mchungaji James David Manning.

Kitendo hiki ni mwendelezo wa mfululizo wa matendo ya kihalifu na ya kibaguzi yaliyofanywa na Lang. Kabla ya tukio hili, alijaribu kuchoma moto Qur’an huko Dearborn, Michigan , mji ambao una idadi kubwa ya Waislamu na Wamarekani wenye asili ya Kiarabu.

Lang, ambaye ni mtu mashuhuri katika mrengo wa kulia wa Marekani, alikuwa amekabiliwa na mashtaka 11 ya shirikisho, ikiwemo shambulio dhidi ya afisa wa polisi na kuvuruga amani, kutokana na jukumu lake katika shambulio la Januari 6, 2021, katika jengo la US Capitol. Hata hivyo, Rais Trump alimpa msamaha katika siku yake ya kwanza ofisini mnamo Januari 2025, kama sehemu ya msamaha mpana kwa wale waliohukumiwa katika kesi hiyo ya Januari 6.

Tangu kuachiliwa kwake, Lang ameongeza kasi ya vitendo vyake vya uchochezi na maandamano ya chuki. Mnamo Februari 2026, alikamatwa baada ya kuharibu sanamu ya barafu iliyokuwa mali ya kundi la maveterani katika jengo la Capitol huko Minnesota. Hivi sasa, anajaribu kujiingiza katika siasa rasmi, akitangaza kugombea kiti cha Seneti ya Marekani kutoka jimbo la Florida.

Vitendo vya karibuni vya Lang, ikiwemo uvunjaji wa heshima wa Qur’an na misimamo yake dhidi ya Uislamu, vimezua malalamiko makali. Vyombo vya habari nchini Marekani vimemwelezea kama mtu mwenye tabia ya uchochezi ambaye anaendeleza harakati zake zenye utata baada ya kupata msamaha wa rais.

3498925

Habari zinazohusiana
captcha