IQNA

15:03 - September 07, 2026
Habari ID: 3482734

Mashindano ya Qur’an ya Kitaifa ya ‘Safir’ yahitimishwa katika Msikiti wa Kufa

IQNA – Toleo la 15 la Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani ya “Safir” limehitimishwa rasmi katika Msikiti Mkuu wa Kufa nchini Iraq.

SAFIR

Mashindano hayo yalijumuisha nyanja za kuhifadhi (Hifdh) na usomaji (Qira’a) wa Qur’ani Tukufu, kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Astan (Usimamizi wa Haram) ya Imam Ali (AS).

Alaa Mohsen, Mkurugenzi wa Kituo cha Dar-ul-Qurani Al-Karim cha Astan hiyo, alieleza kuwa mashindano haya yaliwakutanisha idadi kubwa ya wahifadhi na wasomaji wa Qur’ani Tukufu kutoka taasisi na mashirika mbalimbali nchini humo, wakichuana kwa ustadi wa hali ya juu katika fani za kuhifadhi na kurejea aya tukufu.

Aliongeza kuwa Mohammad Mustafa Qatad Hosseini, ambaye ni msomaji (Qari) na muadhini wa Astan akiwakilisha Kituo cha Dar-ul-Quran, alifanikiwa kutwaa nafasi ya tatu katika mashindano hayo.

Mohsen alihitimisha kwa kubainisha kuwa ushiriki huo ulikuwa sehemu ya mikakati endelevu ya kituo hicho ya kuendeleza na kulea vipaji vya Qur’ani, kuwapa motisha wasomaji, na kuimarisha uwepo wa taasisi hiyo katika mashindano ya kitaifa ya Qur’ani.

3498932

captcha