IQNA – Toleo la saba la mashindano ya kuhifadhi Qur’ani kwa ajili ya wanafunzi wa kimataifa wanaosoma nchini Misri limepangwa kufanyika baadaye mwezi huu.
Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu nchini Misri limetangaza mashindano hayo, ambayo yanawalenga wanafunzi wa kimataifa wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar na vyuo vikuu vingine pamoja na taasisi za elimu ya juu nchini humo.
Mashindano hayo yatafanyika kwa siku tatu, kwa kuanzia Septemba 14 hadi 16, katika makao makuu ya Baraza hilo jijini Cairo, yakifuata ratiba maalum ya washiriki, kama lilivyoripoti gazeti la Al-Ahram.
Hafla hii imeandaliwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu wa kuwasaidia wanafunzi wa kimataifa, kuhimiza kuhifadhi Qur’ani Tukufu, kukuza fikra za wastani na zenye nuru, na kuimarisha uhusiano wa wanafunzi na Qur’ani kupitia kuhifadhi, kutafakari, na kuifanyia kazi katika maisha yao.
Mashindano haya yamegawanywa katika vipengele vitatu: kuhifadhi Qur’ani nzima, kuhifadhi nusu ya Qur’ani, na kuhifadhi robo ya Qur’ani Tukufu.
Zawadi nono za fedha taslimu pamoja na makusanyo ya kitaaluma yaliyochapishwa na Baraza hilo yameandaliwa kwa ajili ya washiriki watakaoshika nafasi za juu.
Aidha, washindi wa kwanza katika kipengele cha kuhifadhi Qur’ani nzima watateuliwa kushiriki katika Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani yatakayoandaliwa na Wizara ya Awqaf ya Misri, yanayotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
3498996
Zenye maoni mengi zaidi