IQNA

Shakhsia wa Qur’ani wa Iran wamtembelea askari aliyepoteza mikono na miguu katika shambulio la kigaidi la Marekani na Israel

IQNA Kundi la viongozi na shakhsia wa jamii ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamemtembelea Hossein Mohammadi, mwanachama wa Vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyepoteza mikono na miguu yake miwili katika shambulio la kichokozi la Marekani na utawala wa Kizayuni wakati wa vita vya siku 40 vilivyotokea mapema mwaka huu.

Mohammadi na mke wake, ambao ndoa yao ilifungwa katika eneo takatifu la makaburi ya mashahidi katika mji wa Kermanshah ulioko magharibi mwa Iran, walikuwa wameweka ahadi wakati huo kuwa “wenza katika uwanja wa mapambano” ili kufikia malengo ya juu ya kiubinadamu na kimaadili, badala ya kuwa mume na mke wa kawaida pekee.

Wawili hao wamebaki waaminifu kabisa kwa ahadi hiyo takatifu hata baada ya askari huyo shujaa kutoa mhanga mikono na miguu yake yote miwili kwa ajili ya kulinda nchi yake ya asili na heshima ya Umma wakati wa mashambulizi yaliyofanywa na adui wa Marekani na utawala wa Kizayuni.

.