IQNA

22:08 - September 14, 2026
Habari ID: 3482771

Kuvunjiwa heshima kwa Qur’ani Tukufu nchini Italia kwazua mawimbi ya malalamiko

IQNA – Kitendo cha kuvunjiwa heshima na kuchomwa moto kwa nakala ya Qur’ani Tukufu kilichofanywa na mwanaharakati mmoja wa kisiasa nchini Italia kimezua ghadhabu na mawimbi ya malalamiko miongoni mwa jamii za Waislamu nchini humo.

i

Utarajiwa na kuchomwa moto kwa nakala ya Qur’ani Tukufu na mwanaharakati huyo wakati wa matangazo ya moja kwa moja kumesababisha hasira kubwa na hatua za kupinga kutoka kwa jamii ya Wamoroko, Umma wa Kiislamu, pamoja na wanaharakati wa mashirika ya kiraia nchini Italia.

Kufuatia tukio hilo la kichokozi, wito umetolewa wa kutaka kuwepo kwa jibu la busara na la kiwajibikaji linalojiepusha na hisia za kukurupuka au kutumbukia katika mtego wa uchochezi uliopangwa, kulingana na ripoti ya shirika la habari la Heba Press.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa barua ya wazi iliyoelekezwa kwa vyombo vya habari na umma kwa ujumla imesisitiza kuwa ukiukaji na kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini hauwezi kamwe kuwa msingi halali wa kuchochea chuki au migawanyiko katika jamii.

Barua hiyo imeweka msisitizo juu ya ulazima wa kutofautisha kati ya “uhuru wa kutoa maoni” na kauli au vitendo vinavyochochea chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) au kudhalilisha kimakusudi itikadi za kidini.

Imetoa wito kwa taasisi za kisiasa na kijamii kubeba dhamana zao katika kupiga vita utoaji wa kauli za chuki na kuacha kutumia vibaya masuala ya kidini kwa ajili ya kujipatia mafanikio ya kisiasa au ya kihariri. Vyombo vya habari navyo vimehimizwa kuchukua mtazamo wa kitaalamu na wa kiwajibikaji wakati wa kuripoti matukio kama hayo ili kuzuia kuongezeka kwa taharuki au kueneza simulizi zinazogawa jamii.

Waanzilishi wa wito huo wamesisitiza kuwa jibu dhidi ya vitendo hivyo sharti libaki kuwa la amani, la kistaarabu, na linalozingatia mipaka ya sheria, huku jitihada za kiraia za kuimarisha mazungumzo kati ya mataifa na dini mbalimbali, pamoja na kutetea thamani za kiustaarabu na heshima ya pande zote, zikiendelea.

Wito huo unasisitiza misingi kwamba kuhifadhi maisha ya pamoja kwa amani na utulivu wa kijamii kunahitaji kukabiliana na uchochezi pamoja na kauli za chuki kwa kutumia busara na uwajibikaji, badala ya kujiingiza katika taharuki zaidi na migawanyiko.

3499015

Habari zinazohusiana
captcha