IQNA

14:56 - September 21, 2026
Habari ID: 3482799

Mwanazuoni Mkuu wa Kishia, Ayatullah Shobeiri Zanjani, aaga dunia

IQNA – Ayatullah al-Udhma Seyed Mousa Shobeiri Zanjani, mwanazuoni mashuhuri wa kidini (Marjaa Taqlid wa Madhehebu ya Shia), amefariki dunia.

zanjani

Ofisi ya mwanazuoni huyo mkuu imesema katika taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo kwamba, roho tukufu ya Faqihi (mwanasheria) wa Ahl-ul-Bayt (amani iwe juu yao) na Marjaa Taqlid mashuhuri wa Kiislamu duniani kwa wafuasi wa madhehebu ya Shia, Ayatullah al-Udhma Seyed Mousa Shobeiri Zanjani, imerejea kwa rehema za Mwenyezi Mungu.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa maisha ya baraka na taaluma tukufu ya kiongozi huyo yamejawa na umahiri mkubwa, jitihada endelevu za kielimu, juhudi za dhati za kuhifadhi na kuinua sheria tukufu (fiqhi), uenezaji wa mafundisho ya Kiislamu, ulinzi wa imani ya Kishia, pamoja na roho ya upendo na huruma kwa jamii.

Wakati ikitoa rambirambi zake kwa msiba huu mkubwa kwa Imamu wa Zama (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), pamoja na kwa vyuo vikuu vya Kiislamu (Hawza), wananchi watukufu wa Iran, na wafuasi wa uongozi wa Kiislamu kote duniani, ofisi hiyo imesema kuwa maelezo zaidi kuhusu shughuli za mazishi ya mwanachuoni huyo mkuu yatatangazwa baadaye.

Ayatullah al-Udhma Shobeiri Zanjani alilazwa hospitalini jijini Qom mnamo jioni ya Ijumaa, Septemba 18, kutokana na maradhi ya mapafu.

3499106

captcha