IQNA

15:42 - September 21, 2026
Habari ID: 3482802

Usajili Wafunguliwa kwa Mashindano ya 22 ya Qur’ani ya Hashimiyya kwa wanawake nchini Jordan

IQNA – Usajili kwa ajili ya duru ya kwanza ya Mashindano ya 22 ya Hashimiyya ya Kuhifadhi na Kusoma Qur’ani Tukufu kwa wanawake umeanza nchini Jordan.

j

Wizara ya Awqaf, Mambo ya Kiislamu na Maeneo Matakatifu ya Jordan imetangaza rasmi siku ya Jumapili kuwa imefungua milango ya usajili kwa mashindano hayo.

Katika taarifa yake, wizara hiyo imewahimiza waombaji wanaovutiwa kukamilisha usajili wao ndani ya muda uliopangwa, ikibainisha kuwa maswali yoyote yanaweza kuelekezwa kwa Kurugenzi ya Masuala ya Wanawake kupitia nambari ya simu (06/5626260).

Maombi yameanza kupokelewa kuanzia Jumatatu hii hadi tarehe 1 Oktoba, yakifanyika kupitia kiungo kinachopatikana kwenye tovuti ya Wizara hiyo au kwa kutumia msimbo wa QR (QR code).

Mashindano hayo yanajumuisha vipengele saba, kikiwemo kile kikuu cha kuhifadhi Qur’ani Tukufu nzima (Juzuu 30).

Wizara imefafanua kuwa vipengele vingine vinahusu kuhifadhi juzuu 25, 20, 15, 10, na 5, hadi kufikia juzuu moja, huku vigezo maalum vya umri vikiwekwa kwa washiriki katika kila ngazi.

Kuhusu vigezo vya ushiriki, mwombaji lazima awe na umri usiopungua miaka 30 ili kushiriki katika kipengele cha kwanza (kuhifadhi Qur’ani nzima), huku umri wa chini kabisa unaohitajika kushiriki katika shindano la juzuu moja ukiwa ni miaka 8.

Duru za mchujo zitafanyika katika mikoa mbalimbali, zikianza Amman, Madaba, wilaya ya Dhiban, na Balqa, na kuhitimishwa Karak na Tafilah. Duru hizo zimepangwa kufanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 mchana (saa za Jordan).

/3499102

captcha