IQNA

17:47 - October 02, 2026
Habari ID: 3482848

Jimbo la California latambua rasmi sikukuu za Kiislamu

IQNA – Jimbo la California nchini Marekani limetambua rasmi Idd al Fitr na Idd al-Adha, sikukuu mbili kuu za kidini katika Uislamu, kufuatia sheria iliyotiwa saini na Gavana Gavin Newsom. Hii ni hatua muhimu kuelekea utambuzi zaidi wa jumuiya za Waislamu katika jimbo hilo.

c

Mswada wa Bunge namba 2017, uliotiwa saini kuwa sheria Jumapili, unaongeza sikukuu hizo katika kalenda rasmi ya sikukuu za jimbo hilo.

Idd al-Fitr huashiria mwisho wa Ramadhani, mwezi mtukufu wa mfungo wa Kiislamu. Idd al-Adha huadhimishwa wakati wa ibada ya kila mwaka ya Hijja.

Shule za umma na vyuo vya jamii vinaweza kufungwa wakati wa sikukuu hizo mbili kupitia taratibu zilizopo za eneo husika. Wafanyakazi wa serikali wanaostahiki pia wanaweza kupata stahiki za sikukuu hizo.

“Kuteuliwa kwa Idd al-Fitr na Idd al-Adha kama sikukuu za jimbo ni uamuzi wa kalenda ya kiraia unaotambua umuhimu wake wa kiutamaduni kwa jamii za California,” kulingana na sheria hiyo.

Sheria hiyo, iliyoletwa mwezi Machi na Mbunge wa Jimbo, Matt Haney, kwa uratibu na makundi na mashirika ya kijamii ya Waislamu, inalenga kurahisisha Waislamu kuadhimisha sikukuu za Iddi bila kukabiliwa na migogoro shuleni au kazini.

Haney alisema kuwa kutambua sikukuu hizo kunaakisi umuhimu wa idadi ya Waislamu wa California na kutawaruhusu familia kusherehekea bila mizigo isiyo ya lazima ya kielimu au kikazi.

Hatua hiyo pia inawapa shule na maeneo ya kazi ya umma mfumo wa kuwezesha maadhimisho ya Iddi hizo mbili za Waislamu.

3499228

captcha