IQNA

17:57 - October 02, 2026
Habari ID: 3482849

Shahidi Nasrallah alidhihirisha sifa ya Qur’ani ya ‘Wenye Nguvu Mbele ya Makafiri, na Wenye Kuhurumiana Wao kwa Wao’

IQNA – Binti ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alizungumza kumhusu baba yake katika maadhimisho ya pili ya kuuawa kwake shahidi.

Zeynab Nasrallah

Akisisitiza tabia na njia ya maisha ya baba yake, Zeynab Nasrallah alisema, “Tulikulia katika shule ya Sayyid Hassan Nasrallah. Hakuwa kiongozi wa kisiasa pekee, bali alikuwa baba kwa watu wote—hususan familia za mashahidi na watu wa kusini mwa Lebanon.”

Alitoa kauli hizo katika mahojiano na kipindi cha Qadiyat Sakhina cha Mtandao wa Kimataifa wa Al-Kawthar.

Alibainisha kuwa kuondoka kwa Sayyid Hassan Nasrallah ni pigo kubwa maradufu kwa familia yake. “Kama ilivyo kwa wengine, tunaomboleza kuondoka kwake; lakini zaidi ya hapo, tumepoteza baba na nguzo ya familia yetu..”

Akirejelea nasaha za baba yake za kila mara, alisema, “Sayyid hakuwahi kubagua kati ya familia yake na umma. Alitoa ushauri uleule kwa kila mtu: kujali watu, kuhifadhi utakatifu na heshima, na kusimama imara katika misingi ndizo zilikuwa mapendekezo yake muhimu zaidi.”

Akisisitiza kuwa “huzuni hii haitatugeuza kutoka kwenye njia ya Muqawama,” aliongeza, “Leo, tumekusanyika chini ya kaulimbiu ‘Tunasimama na Agano’—ahadi iliyotolewa kwa Nasrallah ambayo itadumu kupitia damu ya mashahidi na ahadi yetu imara kwa itikadi za Muqawama hadi pumzi yetu ya mwisho.”

Akirejelea jinai za utawala wa Kizayuni na tukio la milipuko ya vipokezi (pagers), Zeynab Nasrallah alisema, “(Nasrallah) aliumia sana wakati wa tukio hilo, lakini halikumdhoofisha; badala yake, lilimpa nguvu na motisha zaidi. Alidhihirisha sifa ya Qur’ani ya: ‘Wenye nguvu mbele ya makafiri, na wenye kuhurumiana wao kwa wao’—hakubabaika mbele ya maadui, lakini alijawa na upendo na huruma kwa watu na Mujahideen.”

Akizungumzia hali ya sasa nchini Lebanon na kanda hiyo, alisema, “Leo, zaidi ya wakati wowote, tunahitaji utulivu na umoja. Kama Sayyid Hassan Nasrallah alivyosema kila mara, ni lazima tugeuze vitisho kuwa fursa. Shukrani kwa Muqawama na uthabiti wa watu, tuko kwenye njia sahihi, na ushindi wa mwisho ni wa watu wa haki na Muqawama.”

3499247

Habari zinazohusiana
captcha