IQNA – Mamia ya watu wamefanya maandamano jijini Milan kupinga mswada tata wa kupinga Uyahudi (antisemitism) unaojadiliwa katika bunge la Italia, huku makundi ya Wayahudi yakiungana na wito wa kuukataa mswada huo.
Mswada huo, unaojulikana kama DDL 1004, uliwasilishwa na chama cha mrengo mkali wa kulia cha League, ambacho ni mshirika mdogo katika serikali ya mseto ya Waziri Mkuu Giorgia Meloni.
Mswada huo unalenga kutumia vigezo vilivyopitishwa na Muungano wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Holocaust (IHRA) kufafanua kile kinachotajwa kama chuki dhidi ya Uyahudi (antisemitism). Baada ya kupitishwa katika Seneti mwezi Machi, mswada huo sasa uko mbele ya Baraza la Manaibu kwa ajili ya idhini ya mwisho.
Mamia ya waandamanaji walikusanyika Milan wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa “Hapana kwa mswada wa kupinga Uyahudi,” “Kuikosoa Israel siyo chuki dhidi ya Uyahudi,” na “Kuandamana ni haki,” huku wakiimba “Palestina Huru.”
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina, Francesca Albanese, pia amesema kuwa anatumai Waitaliano watapinga sheria hiyo mpya yenye utata mkubwa.
“Kwa nini utamaduni wa Israel ufundishwe nchini Italia??” aliandika Albanese kwenye mtandao wa X akirejelea mswada huo unaojadiliwa bungeni.
Alisema kuwa hatua hiyo ni “sehemu ya mchakato wa kuifanya jamii kuwa ya Kizayuni (Israelization), jambo ambalo wasomi wa serikalini (na sehemu ya wapinzani) wanaliunga mkono.”
“Natumai watu wa Italia watapinga aibu hii inayotangazwa. Historia ni sisi,” aliongeza Albanese.
349925