IQNA

18:38 - October 03, 2026
Habari ID: 3482852

Wanawake wanne miongoni mwa mashahidi katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza

IQNA – Wapalestina watano, wakiwemo wanawake wanne, wameuawa shahidi na wengine kujeruhiwa kufuatia vikosi vya uvamizi vya Israel kulipua ghorofa moja ya makazi magharibi mwa Jiji la Gaza siku ya Jumamosi.

m

Vyanzo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa ndege za kivita za wavamizi  Waisraeli zilipiga ghorofa ya chini ya jengo la “Al-Asala,” magharibi mwa Jiji la Gaza, na kusababisha mashahidi watano na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Vyanzo hivyo viliongeza kuwa vikosi vya ambulensi na uokoaji viliwasafirisha mashahidi na majeruhi hadi hospitalini, huku shughuli za utafutaji wa majeruhi na wahanga wengine waliopoteza maisha chini ya vifusi zikiendelea.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, hadi kufikia Alhamisi, ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji vita na Israel umesababisha mashahidi 1,439 na majeruhi 5,052 wa Kipalestina.

Tangu Oktoba 8, 2023, Israel imeua shahidi zaidi ya Wapalestina 74,000 na kuwajeruhi zaidi ya 175,000 katika Ukanda wa Gaza, kulingana na takwimu za Kipalestina, huku takriban 90% ya miundombinu ya eneo hilo ikiwa imeteketezwa.

3499255/

captcha