IQNA

18:51 - October 03, 2026
Habari ID: 3482853

Mwalimu wa Qur’ani wa Iran aonya kuwa athari za sauti za kidijitali zinahatarisha usomaji wa kijadi

IQNA – Mwalimu maarufu wa Qur’ani kutoka Iran ameonya kuwa ongezeko la matumizi ya vyombo vya muziki na athari za sauti za kidijitali katika usomaji wa Qur’ani ni jambo linalohatarisha uhalisia wa turathi hiyo ya kitamaduni na kidini.

Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya wasomaji wa Qur’ani na Maddah (wasomaji wa qasida Ahlul Bayt AS na qasida za maombolezo) nchini Iran wameanza kuongeza muziki wa ala. muziki wa kielektroniki, na athari za sauti zinazozalishwa na kompyuta chini ya uigizaji wao wa sauti. Mtendo huo umezua mtawanyiko katika jamii ya Qur’ani, huku baadhi wakiuona kama ubunifu na wengine kama tishio kwa taaluma hii tukufu.

Seyed Mohsen Mousavi Baladeh, mwalimu wa Qur’ani na mwandishi wa kitabu Hilyat al-Quran, amekuwa akizungumza waziwazi kuhusu suala hilo, akionya dhidi ya vitendo kama hivyo. Kampeni ya ukusanyaji sahihi imezinduliwa na wafuasi wake kuunga mkono msimamo wake. Alieleza hofu yake katika mahojiano na Shirika la Kimataifa la Habari za Qur’ani  (IQNA).

Mousavi Baladeh anaweka msimamo wake wa kupinga jambo hili na kuongeza kuwa kuwa Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu akiwa na mwili na nafsi, na kwamba muziki ni chakula muhimu kwa ajili ya nafsi.

“Mwenyezi Mungu ameweka chakula maalumu kwa ajili ya nafsi hii, na mojawapo ya vyakula muhimu zaidi ni muziki,” alisema. “Wanadamu hawawezi kufikia usawa bila muziki.”

Anabainisha kuwa usomaji wa Qur’ani wenyewe unatimiza hitaji hili. Anaeleza kuwa lugha ya Kiarabu ya Qur’ani imepangwa kwa takriban thuluthi moja ya herufi “nzito” (zenye kusisitizwa) na thuluthi mbili za herufi “nyepesi”, muundo uliokusudiwa unaounda sifa ya asili ya kimuziki hata inaposomwa bila mahadhi maalumu.

“Wakati usomaji wa kimahadhi wa qari mahiri unapoungana na muundo huu, nuru juu ya nuru huundwa,” alisema. “Mtume Mtukufu (SAW) amesema: ‘Yule ambaye hasomi Qur’ani kwa mahadhi sio miongoni mwetu.’ Hili ni agizo la kimkakati ili hitaji hili la kisaikolojia litimizwe kwa njia ya afya.”

Wasiwasi mkuu wa Mousavi Baladeh ni kwamba kuongeza muziki wa bandia katika usomaji kutaharibu ladha za wasikilizaji. Anaonya kwamba hadhira itazoea sauti hiyo iliyoongezwa na hatimaye kuona usomaji safi, hata ule wa qari wakubwa kama vile Abdul Basit Abdul Samad wa Misri, kuwa wa kuchosha au usio na ladha.

“Matokeo yake ni kwamba usomaji safi wa mabingwa wakubwa kama vile Abdul Basit au qari wetu mashuhuri utaonekana hauna ladha na unachosha kwa kizazi kipya,” alisema.

3499256/

Habari zinazohusiana
captcha