Jumbe zake zinajumuisha masuala mbalimbali, kuanzia kulinda imani binafsi na maadili mema, hadi kusimama imara mbele ya masaibu, kuwa na matumaini ya kupata rehema za Mwenyezi Mungu, uwajibikaji wa kijamii, kuepuka mghafala, na kuelekea katika njia ya haki.
Kwa kuteua aya zenye maudhui maalumu, mfululizo wa “Ujumbe wa Wahyi” unalenga kujenga fungamano linalogusika kati ya maana tukufu za mafunuo na maisha ya kila siku ya hadhira ya leo, na unawasilisha kila aya kama ujumbe wenye kutia moyo, kuzindua fikra, na unaoweza kutekelezwa kiutendaji na walengwa.
Aya hizi zinachapishwa kwa lengo la kueneza utamaduni wa kutafakari na kuzingatia Qur’ani (tadabbur), kuimarisha busara na matumaini, pamoja na kuangaza maisha ya mtu binafsi na ya kijamii, ili kuweka msingi thabiti wa mwamko zaidi, kurekebisha tabia, na kufuata njia ya uongofu wa Mwenyezi Mungu.
Aya ya leo ni aya ya 54 ya Surah Al-An’am: Mola wenu Mlezi amejilazimisha (ameiwajibisha) rehema
