IQNA

17:53 - October 04, 2026
Habari ID: 3482859

Kanisa la Orthodox la Serbia laonya kuwa Wakristo nchini Palestina wanakabiliwa na dhuluma

IQNA – Kanisa la Orthodox la Serbia limesema kuwa Wakristo nchini Palestina wanakabiliwa na dhuluma na ubaguzi, likionya dhidi ya majaribio ya kupuuza au kutenga uwepo wao wa kihistoria.

s

Katika barua kwa afisa wa Palestina, Ramzi Khouri, Patriaki wa Serbia, Porfirije, alionyesha mshikamano na watu wa Palestina, pamoja na kuelezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya inayowakabili Wakristo na wakazi wengine katika eneo hilo.

Khouri ni mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO), na anaongoza Kamati ya Juu ya Rais ya Masuala ya Kanisa nchini Palestina.

Kanisa hilo limesema kuwa jamii hiyo inakabiliwa na “mateso, dhuluma, na ubaguzi,” likisisitiza kuwa mateso ya raia bila kujali imani au asili yao hayaendani na utu wa binadamu.

Lilihimiza kulindwa kwa jamii za Kikristo, likibainisha kuwa Wakristo wamedumisha uwepo endelevu katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 2,000 na wanasalia kuwa sehemu muhimu ya historia na turathi yake.

Kanisa hilo pia lilionya kuwa kuwatenga au kuwadharau jamii yoyote ya kidini au kikabila kuna hatari ya kuharibu mfumo wa kijamii na kidini wa eneo hilo, na lilihimiza kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa na haki za kidini.

Patriaki Porfirije alisema kanisa litaendelea kupaza sauti kuhusu ulinzi wa jamii za Kikristo na juhudi za amani katika Mashariki ya Kati katika mikutano na viongozi wa kisiasa pamoja na taasisi za kimataifa.

Kamati ya Palestina imekuwa ikielezea mara kwa mara wasiwasi wake kuhusu mashambulizi dhidi ya jamii na taasisi za Kikristo katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ikiwa ni pamoja na al-Quds Mashariki inayokaliwa kwa mabavu, pamoja na vikwazo vinavyoathiri ibada, elimu, na ufikiaji wa maeneo matakatifu.

Athari hizo pia zimeenea hadi Ukanda wa Gaza, ambapo Wapalestina watano waliuawa shahidi mapema Jumamosi, wakiwemo wanawake wanne, ambao wawili miongoni mwao walikuwa Wakristo.

3499267

Habari zinazohusiana
captcha