IQNA – Idara ya usimamizi (Astan) ya Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) mjini Karbala, Iraq, imetangaza utayari wake wa kuwatibu wagonjwa wa Kipalestina bila malipo yoyote.
Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalayi, mwakilishi wa Ayatullah Mkuu Sayyis Ali Sistani na msimamizi wa Haram hiyo tukufu, alitangaza utayari wa hospitali na vituo vya afya vinavyofungamana na idara hiyo kupokea na kuwatibu wagonjwa wa Kipalestina bure, pamoja na kugharamia kikamilifu matibabu na usafiri wao.
Katika mkutano na mmoja wa wagonjwa wa Kipalestina anayetibiwa katika vituo vya matibabu vya Haram hiyo, alieleza kuwa gharama zote za matibabu na usafiri kwa ajili ya wagonjwa wa Kipalestina zitatolewa na idara hiyo.
Alibainisha kuwa idara hiyo iko tayari kuwapokea wagonjwa wa Kipalestina katika nyanja mbalimbali za utabibu na maradhi tofauti, na itatoa huduma za afya bila kutoza malipo yoyote.
Mwanazuoni huyo alisisitiza kuwa lengo la hatua hii ni kutoa msaada wa kibinadamu kwa watu wa Palestina katika kipindi hiki kigumu na mazingira mazito wanayokabiliana nayo.
Sheikh al-Karbalayi aliongeza kuwa idara ya usimamizi itaendelea kufuatilia kwa karibu hali za wagonjwa hao hadi pale mchakato wa matibabu yao utakapofikia hatua ya kupona kikamilifu.
Pia alieleza furaha yake kwa kuwakaribisha na kuwahudumia wagonjwa hao wa Palestina.
Hatua hii ni mwendelezo wa shughuli za kibinadamu za Haram hiyo tukufu katika kutoa huduma za afya bila malipo kwa wagonjwa na wenye uhitaji, na inatekelezwa chini ya miongozo na maelekezo ya mwakilishi wa Marja’ Mkuu wa kidini nchini Iraq.
3499269/