IQNA – Wanawake wajitolea kwa ajili ya kazi za katika Msikiti Mtukufu (Masjid al-Haram) mjini Makka wamepata mafunzo katika msikiti huo.
Urais wa Masuala ya Kidini katika Masjid al-Haram na Msikiti wa Mtume (Masjid an-Nabawi) ulitekeleza mpango huo kwa lengo la kuwaimarisha wanawake wajitolea ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanawake wanaozuru Masjid Al Haram.
Mpango huo unalenga kupanua maarifa ya wajitolea kuhusu kazi za uwanjani na kuwafahamisha kuhusu maeneo mbalimbali ya kujitolea, pamoja na kazi na majukumu yanayohusiana nayo. Pia unawaeleza kanuni na maelekezo yanayosimamia kazi hizo, ili kuboresha ubora wa utendaji na kuwaandaa kwa kazi za uwanjani katika Masjid al-Haram.
Mafunzo hayo yalijumuisha vipengele vya kinadharia na vitendo, vikiwemo utangulizi kuhusu maeneo ya kujitolea, kazi na majukumu yaliyopangiwa, pamoja na kanuni na maelekezo husika. Pia yalihusisha mazoezi ya uwanjani, uelekezaji na ufuatiliaji, kwa lengo la kuyageuza maarifa yaliyopatikana kuwa ujuzi wa vitendo unaowezesha utendaji wenye ufanisi.
Kipengele cha kazi za uwanjani kiliimarisha uwezo wa wajitolea na kuwapa uzoefu wa moja kwa moja kwa kuunganisha maarifa na utekelezaji. Aidha, kiliwaandaa kukabiliana na hali na mahitaji ya kazi hizo, kikiunganisha mafunzo ya kinadharia na mazoezi ya vitendo na kuongeza kujiamini pamoja na utayari wao wa kutekeleza majukumu ya kujitolea.
3499284