IQNA – Semina imefanyika nchini Oman kujadili mbinu za kukabiliana na wasiwasi kupitia mafundisho ya Qur’ani Tukufu.
Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kidini ya nchi hiyo, kupitia Kurugenzi Kuu ya Awqaf na Masuala ya Kidini katika Mkoa wa Muscat, iliandaa semina hiyo iliyopewa kichwa cha habari: “Utulivu katika Qur’ani: Kujenga Nafsi katika Zama za Wasiwasi.”
Semina hiyo ya siku mbili ilifunguliwa chini ya ulezi wa Dkt. Rohiya Rashid Al Khaifi, mjumbe wa Baraza la Nchi, ikishirikisha kundi teule la watafiti wanawake na wataalamu katika nyanja za Qur’ani, elimu, na masuala ya kijamii.
Semina hiyo, iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Sultan Qaboos katika Wilaya ya Bawshar, inajadili mada mbalimbali zinazolenga kuimarisha maendeleo ya kiimani na kisaikolojia ya mtu binafsi, kutambua vyanzo vya wasiwasi wa zama hizi, na kubainisha njia za kukabiliana navyo kupitia mwongozo wa Qur’ani, jambo ambalo linachangia kuimarisha utulivu na amani ya kisaikolojia, kifamilia, na kijamii.
3499282