IQNA

19:39 - October 06, 2026
Habari ID: 3482866

Mashindano ya Qur’ani Tukufu kwa Wazee yapangwa jijini Doha

IQNA — Kituo cha Uwezeshaji na Ustawi wa Wazee (Ehsan) nchini Qatar kimetangaza kuanzishwa kwa mashindano ya Qur’ani Tukufu yaliyolenga wazee jijini Doha.

q

Hatua hii inafanyika kama sehemu ya jitihada za kituo hicho katika kuandaa programu na mipango inayojibu mahitaji yao ya kidini, kiutamaduni, na kijamii, huku ikilenga kuboresha maisha yao na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika shughuli za jamii.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, kituo hicho kilieleza kuwa mashindano haya yanalenga kuwahamasisha washiriki wenye umri mkubwa kusoma, kuhifadhi, na kutafakari aya za Qur’ani Tukufu. Vilevile, yanatoa fursa ya kushindana kwa njia chanya katika mazingira ya kiroho yanayoimarisha uhusiano wao na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, huku yakitambua juhudi zao katika kujifunza, kuhifadhi, na ustadi wa usomaji (Tajweed) wa Qur’ani.

Kituo hicho kilisisitiza kuwa mashindano haya ni kielelezo cha dhamira yake ya kutoa programu maalumu zinazokidhi mahitaji na matakwa ya wazee, na kuwahimiza kushiriki katika shughuli za kijamii na kidini. Aidha, inalenga kuibua vipaji bora na kuenzi mafanikio yao, hatua inayoongeza heshima, uwezo, na hisia ya ushirikishwaji na kuthaminiwa katika jamii.

Kituo hicho kilibainisha kuwa mashindano hayo yataendeshwa kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa, kanuni, na vigezo maalum vya kuhukumu ili kuhakikisha uadilifu, uwazi, na usawa kwa washiriki wote.

3499293

Kishikizo: qatar qurani tukufu
captcha