IQNA

Ujumbe wa Wahyi / 6

Mwenyezi Mungu Aamrisha Uadilifu, Wema na Ukarimu

IQNA – Qur’ani Tukufu, Kitabu cha uongofu na uzinduo kwa mwanadamu, inatoa kupitia aya zake jumbe zilizo wazi na zenye kufungua njia sahihi kwa kila zama na kwa watu wote.

Jumbe zake zinajumuisha nyanja mbalimbali: kuanzia kuimarisha imani na maadili ya mtu binafsi, kusubiri na kuwa na ustahimilivu wakati wa mitihani na dhiki, kuwa na matumaini katika rehema ya Mwenyezi Mungu, kutekeleza majukumu ya kijamii, kujiepusha na ghafla, hadi kushikamana imara na njia ya haki.

Mfululizo wa makala za “Ujumbe wa Wahyi” unachagua aya zenye maudhui maalum ili kujenga daraja la uhalisia kati ya maana tukufu za Wahyi na maisha ya kila siku ya walengwa leo. Mfululizo huu unawasilisha kila aya kama ujumbe wenye kutia hamasa, unaozindua fikra na wenye kuweka muongozo wa kiutendaji.

Aya hizi zinachapishwa kwa lengo la kustawisha utamaduni wa kuzingatia na kutafakari Qur’ani (tadabbur), kuimarisha basira na matumaini, na kuangazia maisha ya mtu binafsi pamoja na ya jamii; ili kuweka msingi wa utambuzi mpana zaidi, kurekebisha mienendo, na kuendelea katika njia ya uongofu wa Mwenyezi Mungu.

Aya ya leo ni Aya ya 90 ya Surah An-Nahl:

«إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ»

“Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, na kufanya wema (ihsan), na kuwapa jamaa wa karibu…”

God Commands Us to Be Kind, Generous