IQNA

Ujumbe wa Wahyi

Mada | Ilimu ya Mwenyezi Mungu, yenye kushuhudia kila lahadha ya maisha ya mwanadamu

Qur’ani Tukufu, kitabu cha hidaya na cha kumwamsha mwanadamu, hutoa katika aya zake jumbe zilizo wazi na zenye kuongoza, kwa watu wote na katika zama zote. Jumbe hizo huanzia kuilinda imani na adabu ya mtu binafsi, hadi kusubiri katika shida, kutumainia rehema za Mwenyezi Mungu, kubeba wajibu wa kijamii, kujiepusha na ghafla, na kuendelea katika njia ya haki.

Mfululizo huu wa “Ujumbe wa Wahyi” huchagua aya kwa kufuata mada, kwa lengo la kuunganisha maana tukufu za wahyi na maisha ya wasomaji wa leo. Kila aya huwekwa mbele ya msomaji kama ujumbe wa kutia moyo, wa kuamsha tafakuri, na wa kutumika katika maisha.

فَلَنَقُصَّنَّ عَلَیْهِمْ بِعِلْمٍ وَمَا کُنَّا غَائِبِینَ

Kisha tutawasimulia [zahiri na batini ya itikadi, amali na tabia zao] kwa ilimu [iliyo kamili na yenye kuenea]; [kwani] hatukuwa mbali nao wakati wowote.

Surat Al-A’raf, aya ya 7

Divine Knowledge: Encompassing All Moments of Human Life