IQNA – Shule ya Kiislamu ya Calgary nchini Kanada iliadhimisha Mwezi wa Historia ya Kiislamu mapema wiki hii kwa maonyesho ya urithi yaliyoangazia utamaduni wa Waislamu.
Shule hiyo ya Kiislamu ya Calgary iliandaa maonyesho ya urithi. Wanafunzi walijaza ukumbi wa michezo kwa maonyesho shirikishi.
Wanafunzi hao wamekuwa wakiandaa mradi huo tangu mwanzoni mwa Oktoba, na walisema wanajivunia kuonyesha utofauti wa tamaduni zao kwa jamii na pia kwa wenzao.
“Tunatumaini kwamba watu wataelewa kuwa Waislamu, na hasa Shule ya Kiislamu ya Calgary, wamejaa watu wengi, hadithi nyingi na asili mbalimbali. Tunatumaini watu watakuja kuona kwamba Uislamu ni dini ya tamaduni nyingi, na kila mtu anakaribishwa,” alisema mwalimu Umaiman Samari.
“Hili linatusaidia kuonyesha na kueleza sisi ni akina nani, jinsi tunavyounganisha tamaduni zetu za asili na Uislamu, na jinsi tunavyotumia mafundisho ya Kiislamu kuathiri maisha yetu ya kila siku,” alisema Nuaym Ahmed, mwanafunzi wa darasa la nane.
Oktoba ilitangazwa kuwa Mwezi wa Historia ya Kiislamu na Bunge la Kanada mwaka 2007.
3499620