IQNA – Wanawake wanaojitolea katika Msikiti Mkuu (Masjid al-Haram) katika mji mtukufu wa Makka wanaendelea kuandaliwa kwa kazi za uwandani na utoaji wa huduma msikitini humo.
Idara Kuu ya Masuala ya Dini katika Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume (SAW) inaendelea na mpango wake wa “Dira ya Athari” wa kuwaandaa wanawake wa kujitolea kwa kazi za uwandani na kuboresha huduma kwa wanawake wanaotembelea Msikiti Mkuu.
Mafunzo ya vitendo yaliyofanyika tarehe 26 na 27 Oktoba yaliwatambulisha wajitoleaji 18 kwenye maeneo watakayopangiwa, majukumu yao na miongozo ya kazi, kupitia ziara za utambulisho na mazoezi ya vitendo.
Mpango huo ulipata alama ya jumla ya utendaji ya asilimia 98, huku kiwango cha kuridhika kwa washiriki kikifika asilimia 99.
Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za idara hiyo za kukuza kazi za kujitolea zilizopangwa vizuri na kuimarisha ushiriki wa jamii.
3499618