iqna

IQNA

palestina
Kadhia ya Palestina
IQNA-Viongozi wa Ireland na Uhispania wametangaza kuwa nchi kadhaa za bara la Ulaya zinakaribia kutambua rasmi nchi huru ya Palestina.
Habari ID: 3478676    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/13

Jinai za Israel
IQNA-Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, idadi ya mashahidi wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza imefikia 33,545 huku utawala huo katili ukiendeleza vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo lililozingirwa.
Habari ID: 3478672    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/12

Salamu za Idul Fitr
IQNA-Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, amesema ni wajibu wa kibinadamu na kidini kwa nchi za Kiislamu kukomesha mauaji ya kimbari ya miezi kadhaa ya utawala wa Israel dhidi ya Wa palestina huko Gaza.
Habari ID: 3478661    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/10

Qur'ani na Palestina
IQNA - Programu khitma ya Qur'ani zilifanyika Jumatatu katika shule zaidi ya 20,000 nchini Iran na nchi kadhaa duaniani kuwakumbuka mashahidi mabarobaro Wa palestina katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478660    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/09

Siku ya Quds
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema mhimili wa muqawama una uhakika wa kupata "ushindi mkubwa" katika vita vyake vinavyoendelea dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3478636    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/06

Siku ya Quds
IQNA-Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) anasema utawala wa Kizayuni wa Israel utasambaratika hivi karibuni, akibainisha kuwa Marekani inaiunga mkono waziwazi Israel.
Habari ID: 3478634    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/05

Siku ya Quds
IQNA-Mamillioni ya wananchi wa Iran wamejitokeza katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo yamefanyika leo katika miji na maeneo mbalimbali nchini Iran.
Habari ID: 3478633    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/05

Siku ya Quds
IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema siku ya Quds mwaka huu itakuwa uasi wa kimataifa dhidi ya utawala ghasibu wa Israel na kuongeza kuwa: "Utawala wa Kizayuni wa Israel utazabwa kibao usoni kutokana na shambulio lake dhidi ya majengo ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, mapema wiki hii."
Habari ID: 3478630    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/04

Kadhia ya Palestina
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu ni tofauti na miaka iliyopita, na kwamba operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imemweka adui Mzayuni kwenye ukingo wa shimo la mauti.
Habari ID: 3478629    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/04

Siku ya Quds
IQNA - Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyed Hasan Nasrallah ametoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi barabarani Ijumaa ijayo ambayo inaadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Quds.
Habari ID: 3478605    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/30

Waislamu na kadhia ya Gaza
IQNA - Katika Amerika ya Kusini, jamii za Waislamu zinaadhimisha Ramadhani mwaka huu bila mazingira ya sherehe ambayo ni ya kawaida wakati wa mlo wa futari kutokana na mateso huko Gaza, ambapo zaidi ya Wa palestina 32,500 wameuawa tangu utawala wa Israel uanzishe vita eneo hilo Oktoba 7.
Habari ID: 3478603    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/30

Kadhia ya Palestina
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema vikosi vya mapambano ya Kiislamu ya wapigania ukombozi au Muqawama na Wa palestina wote katika Ukanda wa Gaza ndio washindi kwenye medani ya vita na utawala wa Kizayuni wa Israel ni mwangamizaji wa kizazi na akasisitiza kwa kusema: kilele cha kuheshimika na kusimama imara watu wa Gaza na Palestina na kushindwa utawala wa Kizayuni katika vita hivyo vya miezi sita ni tukio na jambo lenye rehma za Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3478598    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/29

Kadhia ya Palestina
IQNA - Wakati utawala haramu wa Israel umeweka vikwazo vya kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji mtakatifu wa al-Quds, zaidi ya waumini 100,000 wa Ki palestina walishiriki katika Swala maalum ya mwezi wa Ramadhani kwenye msikiti huo siku ya Ijumaa.
Habari ID: 3478560    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/23

IQNA- Katika harakati inayoashiria istiqama, Wa palestina katika Ukanda wa Gaza siku ya Ijumaa walishiriki katika sala ya kwanza ya Ijumaa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Machi 15 katika eneo lenye mabaki ya Msikiti wa Rafah ambalo ulibomolewa hivi karibuni katika hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3478527    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/17

Wapalestina katika Mwezi wa Ramadhani
IQNA - Rais wa Jumuiya ya Wahubiri wa Kiislamu Palestina ametoa wito kwa Waislamu wote wanaofunga mwezi mtukufu wa Ramadhani waombe dua kwa ajili kukomeshwa mateso na masaibu wanayokumbana nao watu wa Gaza.
Habari ID: 3478495    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/12

Watetezi wa Palestina
IQNA - Wnawake wanaharakati wanaounga mkono Palestina wameandamana katike eneo la Freedom Plaza katika mji mkuu wa Marekani, Washington, DC, kutangaza mshikamano na wanawake wa Ki palestina wanaoteseka huko Gaza, huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendeleza mauaji ya kimbari katika eneo hilo.
Habari ID: 3478472    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/09

Hali ya Palestina
IQNA - Mashambulio yasiyokoma ya utawala katili wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza uliozingirwa yamewanyima Waislamu duniani furaha ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3478469    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/08

Jinai za Israel
IQNA - Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake hii leo, ofisi ya vyombo vya habari vya serikali huko Gaza imeomboleza wanawake 8,900 wa Ki palestina waliouawa tangu Oktoba wakati utawala katili wa Israel ulipoanza mauaji ya kimbari dhidi ya Wa palestina katika eneo hilo.
Habari ID: 3478468    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/08

Kadhia ya Palestina
IQNA - Utawala wa Kizayuni wa Israel unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina umetangaza siku ya Jumanne kwamba utawaruhusu waumini kuingia katika Msikiti wa al-Aqsa katika eneo la Quds (Jerusalem) katika wiki ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani, na hivyo kutupilia mbali mpango wa awali wa kuweka vizuizi.
Habari ID: 3478461    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/06

Kadhia ya Palestina
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepanda mzeituni katika hatua ambayo ameitaja kuwa ni mshikamano na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
Habari ID: 3478453    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/05