IQNA

Maonyesho ya Qurani na kaligrafia ya Kiislamu yaanza Georgia Marekani

16:17 - August 28, 2010
Habari ID: 1982861
Maonyesho ya Qurani na kaligrafia ya Kiislamu yameanza Agosti 28 hadi Desemba 5 katika jimbo la Georgia.
Kwa mujibu wa tovuti ya carlos.emory.edu maonyesho haya yatakayofanyika katika Jumba la Makumbusho la Emory Carlos yatajumuisha sanaa za Kiislamu za karne za 1600-1900 Miladia na yatajumuisha sanaa za Qurani na kaligrafia za Kiislamu kutoka maeneo ya Uhispania na Kaskazini mwa Afrika. Maonyesho hayo yatakuwa na nuskha 20 za Qurani Tukufu kutoka maeneo mbali mbali duniani. Imearifiwa kuwa vile vile kutakuwa na athari 150 za sanaa pamoja na vifaa vya kaligrafia. Athari hizo zimetoka nchi kama vile Iran, Uturuki, India na meneo mengine.
642988
captcha