Kisimamo cha Arafa kinahesabiwa kuwa moja ya nguzo muhimu kabisa za ibada ya Hija na kama ilivyonukuliwa katika riwaya ni kwamba, atakayepitwa na kisimamo cha siku ya tarehe 9 Dhil Hijja katika uwanja wa Arafa basi atakuwa hana Hija.
Mahujaji wanatarajiwa kukipitisha kipindi chote cha mchana wakiwa katika uwanja huo wa Arafa wakiomba dua na baada ya kuzama jua wataelekea Muzdalifa.
Aidha leo mahujaji kutoka nchi mbalimbali wameungana na mahujaji wa Kiirani kwa ajili ya kutekeleza marasimu ya kujibari na kujiweka mbali na washirikina katika jangwa la Arafa sambamba na kusomwa ujumbe wa hija ya mwaka huu wa Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. 695903